Thursday, October 9, 2014

Picha:Tazama Jinsi Wajumbe wa Bunge Maalum La Katiba Walivyoserebuka Jana Wakati Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Walivyokabidhiwa Rasmi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Mjini Dodoma


 Mbunge wa Maswa John Shibuda, akijumuika na wasanii wa ngoma ya asili kutoka Mkoa wa Shinyanga kusebeneka...
 Martha Mrata na Mageth Sita wakifurahia wakati wakiserebuka katika sherehe hizo.
 Wajumbe wakirudi jukwaani....
 Mrema akiungana na wajumbe wenzake kusherehekea.....
  Wajumbe wakiserebuka
 Wajumbe wakirudi jukwaani....
 |Serebuka....
 Kila mmoja alikuwa na furaha teleee.....
 Mrema akiungana na wajumbe wenzake kusherehekea.....
 Mbunge wa Maswa John Shibuda, akijumuika na wasanii wa ngoma ya asili kutoka Mkoa wa Shinyanga kusebeneka...
  Wasanii wa bendi ya TOT Taarab wakishambulia jukwaa.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
source: haki ngowi

RAIS KENYATTA APOKEWA KWA SHANGWE NAIROBI

Makundi ya watu wanaoshangilia, yamempokea Rais Uhuru Kenyatta ambaye amerejea Kenya baada ya kuhudhuria Mahakama ya Kimataifa ICC, iliyopo The Hague.
Bwana Kenyatta alihudhuria shauri mahakamani siku ya Jumatano, na kuwa rais wa kwanza aliyepo madarakani kufika katika mahakama ya ICC.


Anakanusha mashtaka dhidi yake ya uhalifu dhidi ya ubinaadam kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zilizosababisha vifo vya watu 1,200 na wengine 600,000 kupoteza makazi.

Rais Kenyatta alipokelewa Nairobi kwa gwaride la heshima na ngoma.


Picha: Bw Kenyatta akiwa na mmoja wa mawakili wake wa utetezi ICC.

source: matukiotz.com

TRAFIKI WA PICHA YA MAHABA WATIMULIWA KAZI

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani walioachishwa kazi.
ASKARI wa Kikosi cha Usalama Barabarani waliopiga picha ya mahaba wakibusiana huku wakiwa wamevaa sare za Jeshi la Polisi na picha yao ikasambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii wamefukuzwa kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe amethibitisha leo kwa waandishi wa habari mkoani humo kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha kulidhalilisha Jeshi la Polisi.
Kamanda Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Misenyi, mkoani Kagera.

source: matukiotz.com