Wednesday, October 31, 2012

UKOSEKANI WA USIMAMIZI MZURI WA MATUMIZI YA FEDHA YA SERIKALI:



  • Kilio cha baadhi ya wabunge kuwa wabunge wengi ni wepesi wa kupanga na kusema lakini kwa ujumla utekelezaji wa mipango hiyo yote ni duni;



  • Tatizo ni nini?



  • Je kunasababu ya kuendelea kukopa nje wakati matumizi ya mikopo hiyo pengine haina tija kwa wananchi ambao ndio wanaotakiwa kulipa madeni hayo?


Karibu mezani tujadili kwa faida ya Taifa letu

KWA KWELI WATOTO HAWA WAMEIMBA KWA UPENDO SANA WIMBO HUU



  • Je sisi kama viongozi wenye mamlaka ya kutimiza ndoto zao ambazo wanazitegemea kupitia wimbo huu ni kweli kuwa tunatekeleza ukweli wa wimbo huu?



  • Inasikitisha kama tunashindwa kutimiza viapo vyetu kwa faida yao



  • Tuwakumbuke watoto hao kwa elimu na maisha yao bora jamani viongozi


Ni wakati wetu wa kuwajibika kwa faida yao na tufanye hivyo

MAMA FATUMA KARUME AONGELEA MUUNGANO;



  • Taifa letu limekuwa katika majadiliano makali sana kuhusu swala la Muungano wa Zanzibar na Tanganyika;



  • Muungano umeibua hisia tofauti na hata kwa upande mwingine chuki miongoni mwa Watanzania



  • Je Muungano bado unamuhimu kwetu kama Taifa?



  • Je swala la Muungano na fujo ambazo pengine zinaendelea hivi sana behind the scene kwa namna tofauti ni lazima ziendelee?



  • Kwani katiba Mpya haiwezi kuleta suluhisho na kuondoa chuki zinazohusiana na swal nzima la matatizo ya Muungano?


hebu tupe mawazo yako; 

Tuesday, October 30, 2012

KWA UTARATIBU HUU MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA NI NDOTO



  • inasikitisha kuona watendaji wa serikali ambao wamechaguliwa na wananchi ili kuwawakilisha kwa ajili ya maendeleo yoa ndo wanawageuka hivi hivi ili kutimiza masilahi binafsi. 



  • Tunatakiwa kuwa makani tupatapo nafasi ya kuwachagua  wawakilishi wetu; kweli tunatakiwa kuwachagua wale ambao watakuwa tayari kutusaidia.


Bado tunasafari ndefu sana;

Hebu msikilize Mwanaharakati Mzee Mkinga kama kawa akichambua utendaji wa serikali yetu



  • Je ni kweli kuwa watendaji wengi wakuu wa serikali maneno yao na vitende vyao halivingani kama mwanaharakati Mkinga navyosema?



  • je nini kifanyike katika kulidhibiti hali hii?


mawazo yetu ya pamoja yanaweza kuleta suluhu ya Tatizo hili hebu tuongee pamoja:

NINI CHANZO CHA MIGOMO TANZANIA?



  • Ni kweli kuwa chanzo cha migomo mingi hapa nchini kwetu inasababishwa na mifumo mibovu ya uendeshaji wa serikali?



  • Migomo imegusa karibu kila eneo la maisha ya Jamii, Je tunawezaje kuepuka hali hii isiendelee tena au sijitokeze mara nyingi?



  • Viongozi wetu wanatambua kuwa pengine chanzo cha migomo ni husababishwa na wao?


Ni wakati mzuri wa kujadili na mwenzako wakati wa mapumziko au mkiwa mnakunywa kahawa

Monday, October 29, 2012

JE KWELI WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI WANATEKELEZA MAJUKUMU YAO IPASAVYO?



  • Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameelezee kwa ufupi utendaji wa serikali na amekubali kuwa kuna changamoto kubwa katika kufikia malengo yalikyokusudiwa kwa wananchi kutokana na sababu tofauti;



  • Je ukiwaangalia mawaziri wetu ni mawaziri gani kweli wanatekeleza majukumu yao kwa dhati kwa faida ya Taifa kwa kiwango cha juu?



  • na kwa wale ambao unafikiri wameshindwa kutekeleza au kusimamia majuku yao kwa kiwango kinachotakiwa nini kifanyike dhidi yao?


Hebu tushirikishe mawazo yako kwa kauli ya Waziri Mkuu kuhusu utendaji wa mawaziri wetu na watumishi wakuu wa serikali;

NI KWELI KUWA CCM INAJIMALIZA YENYEWE?



  • Mheshimiwa Ole Sendeka ametoa mchango mkubwa sana katika hoja yake ambayo ikichukuliwa kwa umakini wake inaweza sana saidia kuimarisha Chama cha Mapinduzi wakati huu wa ushindani mkubwa wa kisiasa;



  • Nina imani kuwa Mheshimiwa Kikwete anaweza kukinusuru chama chake kam kwanza atafanikiwa kuwatambua maadui wa ndani ambao ndio wabaya kuliko maadui wa nje,


wewe unasemaje tujadili?

JE UMASIKINI WA WATANZANIA UNASABABISHWA NA SERIKALI?




  • Mjadala wa nini chanzo cha umasikini wa watanzania ni mjadala ambao unashika kasi hivi sasa;



  • je umasikini wa watanzania  unasababishwa na serikali au wananchi wenyewe?



  • je nini kifanyike kwa haraka ili kuepusha tatizo hili kuendelea kulifanya taifa hili ambalo lina rasilimali nyingi kuendelea kuwa na wananchi masikini?


Hebu nasi tulifikirie na tuendelee kulijadili popote pale ulipo kwa faida ya watanzania

Sunday, October 28, 2012

JE NI KWELI KUWA MHESHIMIWA DR. JOHN POMBE MAGUFULI NI MSIMAMIAJI WA SERA ZA MAENDELEO NA SIO SIASA?



  • Mheshimiwa Magufuli amekuwa akilalamikiwa sana kwa bomoa bomoa kwa wale wote ambao wamejenga ndani ya hifadhi ya barabara; zoezi hili amekuwa akilifanya kulingana na sheria ya barabara hata wakati fulani bosi wake Mheshimiwa Jakaya Kikwete alimpunguza kasi; je kwa kitendo kama hicho cha kupunguzwa kasi  knatufundisha nini sisi kama wananchi?



  • Daima mheshimiwa Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa yeye hataki kuendekeza siasa katika kuwaletea maendeleo wananchi, je katika siasa za bongo na ushindani wa siasa na uombaji wa kura inawezekana?



  • lakini Namwona Magufuli ni baadhi ya watendaji wachache ambao wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kwa hamu ya kuwaletea maendeleo watanzania, japo pengine hatua hii inaumiza kwani anafanya sivyo vile sisi tunavyofanya bali sheria inavyotaka.


wewe unasemaje Njoo tujadili

JE UTEUZI WA VIONGOZI WETU KATIKA NGAZI MBALIMBALI UNAFUATA SIFA GANI



  • Jenerali Ulimwengu anahoja hapa ikiiangalia kwa makini



  • Washauri wa viongozi wetu wa juu wana nafasi gani katika kushauri uendeshaji wa Serikali?



  • Ni kweli kuwa Marekebisho ya katika ijayo itaweza kuliona hili na kulijadili kwa faida na Taifa na sio watu wachache?


Hebu tutathimini hoja hii na tuijadili

UWEZO WA WANASIASA WETU UNAPIMWA KWA KIGEZO GANI WAKATI WA KAMPENI?




  • Kampeni za stahili hii zitaweza kulisaidia Taifa letu katika maendeleo ya wananchi wao?



  • Kiongozi mwenye dhamana ndani ya Chama chake anapofanya kampeni za matusi tutegemee nini?



  • Hata kama aliomba radhi Nafikiri hii itabaki kuwa Legacy ya uongozi wake kwa vizazi vijavyo



  • Nilicheka sana na wakati huu huu nilisikitika sana  na natamani kufahamu CV yake


Hebu Tuijadili tunavyoelekea katika uchaguzi wa mwaka 2015

NI KWELI KATIKA TANZANIA YETU YA LEO WASOMI WAMEWEKA ELIMU YAO MIFUKONI?



  • Mheshimiwa Msigwa pengine ana hoja ya msingi: Je kama anahoja ya msingi kwa nini ushauri wake usifanyiwe kazi?


  • au tunaendekeza sana uhasama wa vyama na sera na siasa zake?


  • naipenda siasa pale tu itakapo weza kuwasaidia wananchi wenye uwezo wa chini na wanaoendelea kuishi katika maisha magumu


Hebu isikilize hii na kisha tuijadili

HII NI KALI LAKINI IMEBEBA UJUMBE MZITO



  • Kilio chake ni cha kweli kabisa kina mengi ya kujifunza 
  • Tusiishie tu kucheka kuna mambo ambayo kweli yanahitaji marekebisho katika soka letu

  • Je soka limegeuka kuwa uhasama au ni huluka yetu sisi mashabiki na soka letu kutishana;

  • Nimecheka sana lakini inauma sana

  • kwa nini amesema kuwa hiyo hali haiwasumbui wachezaji?

Hebu tujadili

Saturday, October 27, 2012

kiongozi wa serikali anaposhemsha engine ya ubongo wake

Picture

source: katuni via GPL

  • Je kiongozi wa namna hii bado ansastahili kuendelea kushika madaraka;

  • Je ni vigezo gani vilitumika kumpa madaraka kama hayuko makini katika kusoma hotuba yake ambayo pengine ameikariri kwa wiki nzima na akachanganywa ubongo kidogo tu na mjumbe aliyemtangulia kutoka zimbabwe kama kweli maelezo ya utetezi wake unakidhi haja.

  • Mheshimiwa Kikwete kazi unayo kama viongozi wetu ndo wako hivi basi tusitegemee maisha bora kwa kila mtu ndani ya muda mfupi.
wadau mnasemaje?