Tuesday, February 25, 2014

Mabomu yalipuka makanisani

 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mkadam Khamis Mkadam.
Watu  wanne wamejeruhiwa katika tukio moja kati ya manne ya milipuko ya mabomu yakiwamo mawili yaliyolipuka eneo la makanisa mawili visiwani hapa.
Katika tukio la kwanza, watu wanne walijeruhiwa baada ya mmoja wao kuokota mabaki ya silaha katika eneo la kufanyia mazoezi ya kijeshi huko Unguja Ukuu katika Wilaya ya Kusini Unguja.

Eneo hilo liko karibu na pwani na hutumiwa na wanajeshi kwa ajili ya kufanyia mazoezi.

Shabani Khamis Ibrahim, mmoja kati ya majeruhi wa tukio la Unguja Ukuu, aliyelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, aliliambia NIPASHE kuwa bomu hilo lililipuka akiwa kwa fundi akitengeneza pikipiki yake.

“Ghafla nilihisi kitu kimenipiga kiunoni na hapo ndipo nilipojihisi kuwa nimeumia na kukimbizwa hospitali,” alisema Shabani.

Majeruhi hao walifikishwa katika hospitali hiyo na watatu hali zao siyo nzuri ingawa mmoja ameruhusiwa.

Majeruhi hao ni Pandu Haji Pandu, Shabani Khamis Ibrahim, Juma Abdallah na Simai Hussein aliyeruhusiwa.

Matukio mengine ya milipuko ya mabomu yametokea katika makanisa mawili na katika mgahawa wa kitalii wa Mercury uliopo Forodhani.

Akizungumza na NIPASHE, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo juzi na jana na kwamba uchunguzi unaendelea.

“Tumefika eneo la matukio na ni kweli kuwa milipuko iliyotokea ni ya mabomu, ila bado hatujajua ni aina gani ya mabomu yaliotumika, hivyo ni mapema mno kusema kwani uchunguzi bado unaendelea,” alisema Kamanda Mkadam.

Matukio hayo yalitokea katika eneo la Mkunazini, Forodhani na Kijito Upele ambako hadi jana jioni hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na matukio hayo.

Mlipuko mwingine ulitokea karibu na Kanisa la Anglikana eneo la Mnara Mmoja saa 7:00 mchana.

Bomu hilo lilichimba barabara, ukuta wa kanisa hilo na kuvunja vioo vya gari moja lililokuwa limeegeshwa eneo hilo.

Mmiliki wa gari lililokuwa limeegeshwa, Mohamed Ibrahim Ali, alisema kuwa aliegesha gari lake eneo hilo na kwenda kuswali, lakini aliporejea na kukuta watu wakiwa wanashangaa mlipuko wa kwanza, aliingia katika gari laki na ghafla ulitokea mlipuko uliovunja vioo na kumsababishia michubuko.

Kamanda Mkadam alithibitisha kutokea kwa mlipuko huo, lakini alisema walichukua vipande vya mlipuko kwa ajili ya uchunguzi.

Vile vile, Kamanda Mkadam alisema juzi asubuhi ulitokea mlipuko nje ya Kanisa la Assemblies of God katika eneo la Kijito Upele, Wilaya ya Magharibi wakati waumini wakiendelea na ibada, lakini haukusababisha athari zozote.

Kuhusu mlipuko uliotokea katika mgahawa wa Mercury uliopo Forodhani, Kamanda Mkadam alisema lilitokea saa 6:00 mchana jana mbele ya mgahawa huo na kuchimba ardhini na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
 
CHANZO: NIPASHE

Saturday, February 22, 2014

MBEYA CITY 0 - 2 COASTAL UNION

timu_kau_blog_cc87a.jpg
Leo mambo yamekuwa magumu kwa Mbeya City baada ya kukubali kufungwa na Coastal Union ya jijini Tanga kwa goli 2 bila

source: mjengwa blog

Nchi changa zapata makadinali kadha

papa_fb437.jpg

Makadinali 19 wepya wa Kanisa Katoliki wametawazwa leo katika sherehe iliyofanywa Vatikani - uteuzi wa kwanza kufanywa na Papa Francis tangu kuchukua uongozi wa Kanisa Katoliki.

Ameteua viongozi wa kanisa kutoka nchi 12 zikiwemo Haiti, Burkina Faso na Ivory Coast ambao walivishwa majoho na kofia nyekundu.

Papa mstaafu, Benedict wa kumi na sita, naye alihudhuria, akionekana kwenye ibada ya hadhara kwa mara ya kwanza tangu kustaafu.

Mwandishi wa BBC Vatikani anasema uteuzi wa makadinali aliofanya Papa Francis unaonesha amebadilisha dira kutoka Ulaya na kuelekea maeneo ambako Kanisa Katoliki lina nguvu, yaani Amerika Kusini na Kati na Afrika.

Na kadinali mwengine mpya ni mkuu wa Kanisa Katoliki la Uingereza naWales, Askofu Vincent Nichol.

Chanzo, bbcswahili.com

Friday, February 21, 2014

Lissu, Lipumba, Werema jino kwa jino bungeni

Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu.
Malumbano, vijembe na mvutano vimeanza kuibuka mapema katika Bunge la Katiba jana, baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kumaliza kutoa elimu na ufafanuzi kwa wajumbe kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, huku Tundu Lissu, akidai kuwa Jaji Werema amefanya upotoshaji mkubwa.
Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, alidai kuwa Jaji Werema alifanya upotoshaji huo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu sheria hiyo kwa wajumbe wa Bunge la Maaluma la Katiba jana.

Akiwa wa kwanza kuuliza swali baada ya Jaji Werema kumaliza kutoa darasa la somo la sheria hiyo kwa wajumbe na ufafanuzi mbalimbali, Lissu alisema, “Napenda kurekebisha upotoshaji uliofanywa na mjumbe.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, kifungu 25 (1) kinasema, ‘Bunge Maalum litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha masharti ya katiba inayopendekezwa, kutunga masharti ya mpito na masharti yatokanayo kama Bunge Maalum litakavyoona inafaa.

“Nguvu za wajumbe wa Bunge la Maalum ipo kwenye hicho kifungu cha 25 na kifungu cha 9 kinahusu kazi za Tume…mamlaka ya Bunge hili yako kwenye kifungu cha 25,” alisema na kuongeza, “Tafadhali tusipotoshane hapa.”

Baada ya hapo, alifuata Zitto Kabwe, aliyehoji kuwa katika sheria hiyo hakuna maeneo hayo ya ukomo ambayo yanahusisha Bunge Maalum la Katiba lakini Jaji Werema amesisitiza sana katika eneo hili.

Pia alitaka kujua baadhi ya makundi ya watu, taasisi na vyama ambavyo vimetengeneza rasimu mbadala za katiba na mamlaka ya wajumbe kuhusu rasimu hizo yapoje kupoea rasimu mbadala.

Kwa upande wake, Mwalimu Ezekiel Oluochi, akitokea kundi la vyama vya wafanyakazi alisema hakuna uhusiano wowote kati ya kifungu cha 9 na kifungu cha 25 cha sheria hiyo.

Naye Hamad Rashid, Mbunge wa Wawi (CUF), alihoji mamlaka ya Bunge hilo iwapo katika rasimu hiyo itaonekana Tume haikufanyakazi yake.

Mjumbe Hamza Hassan Juma, alitaka wajumbe wenzake kujikita zaidi katika sheria hiyo iliyowaleta hapo, na ndio maana waliomba wapewe muda wa kutosha wa kuipitia.

Christopher Ole Sendeka, alisema Bunge hilo halina uwezo wa kujadili masuala ya Jamhuri na ikiwa tofauti na hivyo, uhalali wa Bunge hilo upo wapi.

Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumzia suala la mamlaka na madaraka ya Bunge hilo alilazimika kunukuu maneno ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuwa si suala la kawaida kwa Bunge hilo kunyang’anya madaraka ya wananchi, isipokuwa kuboresha maoni yao.

Baadaye alifuatia Ismail Aden Rage, ambaye awali alijinadi kuwa ni Rais wa Klabu ya Mpira ya Simba, alionekana wazi kumshambulia Profesa Lipumba kwa nukuu alizodai kuwa zimeandikwa kwenye gazeti la Mawio.

Lakini hata hivyo, Musa Haji Kombo alipopata nafasi ya kuuliza swali alimtetea Profesa Lipumba pale aliposema wasomi hutumia nukuu mbalimbali kujenga hoja ili kufikia uelewa na uamuzi mzuri wa hoja zinazobishaniwa.

Bila kumtaja kwa jina alisema, alichofanya Profesa Lipumba ni sahihi kabisa kufanywa na wataalam wengi na sio kama ambavyo wanafanya marais wa vilabu michezo katika uongozi wa timu zao na ndio maana hazina maendeleo.

Mapema akinukuu kifungu cha 9 (2) (a) hadi (i) kinachozungumzia misingi mikuu ya kitaifa na maadili, Jaji Werema, alisema wajumbe hawana mamlaka ya kujadili mambo hayo.

“Sheria imeweka mambo ya kufanya kwa wajumbe kwenye Rasimu ya Katiba hii yale yote mnayoyapenda lakini kuna mipaka…mna mamlaka lakini kuna mipaka, fanyeni mnachotaka, lakini hamuwezi kujadili kuhusu misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii kama ilivyo katika kifungu 9,” alisema.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, mambo ambayo wajumbe hawaruhusiwi kuyabadili ni kuhusu kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano, uwapo wa Serikali, Bunge na Mahakama, mfumo wa kiutawala wa kijamhuri na uwapo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Misingi mingine ambayo hawawezi kubadili ni umoja wa kitaifa, amani na utulivu, uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote wenye sifa ya kupiga kura, ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu, utu, usawa mbele ya sheria na mwenendo wa sheria na uwepo wa Jamhuri ya Muungano isiyofungamana na dini yo yote na inayoheshimu uhuru wa kuabudu.

Akijibu maswali na maoni ya wajumbe, Jaji Werema, alisema, Lissu alisema mamlaka ya Tume ya Warioba hayawezi kutumika katika Bunge hili.

Jaji Werema alitoa mfano wa jongoo ambaye ana miguu mingi, lakini yote inafanya kazi kwa ushirikiano na kumwezesha jongoo kutembea.

“Unaposoma sheria unapaswa kujua unasoma sheria kama  kitabu, kwa njia ambayo inaleta maana, lakini ukisoma sheria kama mstari mmoja wa Bibilia na kutoka nao utapotoka,” alisema.

Alisema misingi mikuu ya taifa imetajwa kwenye kifungu cha 9 (2) na imetumika kwa Tume ya Jaji Warioba na inatumika pia kwa Bunge hilo.

“Mimi nina viapo vinne na sijapotosha hata mara moja,” alisema bila kuvitaja.

Alisema kwenye kutafsiri sheria maneno yaliyomo pembeni kwa sheria (marginal notes), hayasaidii kitu chochote kama ambavyo Lissu alitumia maneno hayo kutoa maelezo yake bungeni. “Kama hali ndiyo hiyo, walimu wa sheria ongezeni bidii,” alisema.

Kuhusu ajenda ya Bunge Maalum, alisema ni Rasimu ya Katiba na siyo rasimu nyingine yoyote ambayo imetengenezwa pembeni, lakini hata hivyo, alisema kama mmoja anaweza kuipata basi asiipige teke, itamsaidia.

Kuhusu hoja iliyotolewa na Profesa Lipumba, alisema, Jaji Warioba hakukosea, ila inategemea mmoja anasoma kama mwanasiasa, mtaalum au mwanasheria.

Alisema maswali mengi ya wananchi ni kwamba wanataka au kuona sio sahihi kwa Bunge kufanya ukarabati wa rasimu hii, kwani wana nguvu ya kuifanyia mabadiliko rasimu hii.

Lakini ukweli ni kwamba bunge hilo halina mamlaka ya kuondoa misingi muhimu ya Katiba, ni kweli ipo katika kifungu cha 9.

Katika hatua nyingine, Jaji Werema aliwaomba wajumbe wavumiliane. “Naomba sana jamani tuvumiliane, wale wote tuliogombana zamani mimi nasema hadharani sasa nimeacha, tukubaliane kufanya kazi,” alisema.

Bunge limeahirishwa hadi Jumatatu, watakapoanza kujadili kanuni ambazo ziliwasilishwa jana bungeni na ofisa wa Bunge, Oscar Mtenda.
 
CHANZO: NIPASHE

Kura ya siri Katiba Mpya

bunge_33282.png

Dodoma. Rasimu za kanuni za uendeshaji Bunge Maalumu la Katiba zimependekeza kutumika kwa utaratibu wa kupiga kura ya siri wakati wa kupata uamuzi wa kupitisha Rasimu ya Katiba.
Endapo mapendekezo hayo yatapitishwa, hoja ya Katiba Mpya itakayowasilishwa na Kamati ya Bunge Maalumu la Katiba, itaamuliwa kwa kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe wa Tanzania Bara na idadi kama hiyo ya wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar
.
Upigaji kura huo kwa siri, umepongezwa na baadhi ya wabunge kwa maelezo kuwa utatoa fursa kwa wajumbe kupiga kura hizo kwa uhuru na bila kushinikizwa na misimamo ya vyama au taasisi zilizowapendekeza.
Kanuni hizo zimekuja wakati CCM, kikiwa kimewaagiza wajumbe wake ambao ndiyo wengi bungeni, kutetea muundo wa Serikali mbili badala ya ule wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Pamoja na CCM kuweka msimamo wa kuwataka wajumbe wake kuutetea mfumo huo, kumeibuka mgawanyiko mkubwa huku baadhi yao wakitarajiwa kukitosa na kuunga mkono mfumo wa Serikali tatu.
Kanuni ya 82(1) ya rasimu hiyo, imeweka bayana kuwa utaratibu utakaotumika kupata uamuzi baada ya mwenyekiti kulihoji Bunge ni wa ama kura ya siri au ya kielektroniki.
"Wakati wa kupiga kura ya siri, kila mjumbe atapiga kura ya Ndiyo au Hapana kwa kutumia karatasi za kupigia kura zitakazokuwa zimeandaliwa na Katibu wa Bunge," inasomeka kanuni ya 83(1).
Kanuni hiyo imeweka wazi kuwa kupiga kura kwa mujibu wa masharti ya kanuni hiyo, itakuwa ni wajibu na haki ya msingi ya kila mjumbe na kwamba kila mjumbe atapiga kura kwa binafsi yake.
Hatua ya wajumbe kupiga kura hiyo, itatanguliwa na kazi ya kila Kamati ya Bunge Maalumu, kujadili rasimu ya katiba hiyo kulingana na mgawanyo wa majukumu. Kamati 17 zitashughulikia ibara za rasimu.
Baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ataagiza taarifa ya kamati iwekwe kwenye orodha ya shughuli kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni kwa mjadala.
Kanuni hizo zimeeleza kuwa wakati wa mjadala huo, mjumbe yeyote anaweza kushauri na kutoa mapendekezo ya marekebisho au mabadiliko kwa ajili ya kuboresha sura ya rasimu inayohusika.
Hata hivyo, Kanuni za 78 (11) na 78 (12) za rasimu hiyo, zinapendekeza mwenyekiti asiruhusu hoja yoyote inayokiuka sheria au pendekezo la kamati linalohusu jambo lililo nje ya mamlaka ya Bunge.
Rasimu hizo za kanuni zimegawanywa kwa wajumbe wote 629 wa Bunge Maalumu la Katiba na kuanzia juzi hadi Jumapili, watakuwa wakizisoma na baadaye kuanza kujadiliwa Jumatatu ijayo.
Akizungumzia upigaji kura kuwa wa siri, Mjumbe wa Bunge Maalumu, Grace Kiwelu alisema utaratibu huo utatoa fursa kwa wajumbe kuwa huru kufanya uamuzi wenye masilahi kwa taifa badala ya vyama.
Mjumbe mwingine, Esther Bulaya naye alisema kanuni hiyo ni mwafaka kwa sababu itawafanya wabunge kupiga kura kwa uhuru na bila kuhofia kwamba chama au taasisi iliyompendekeza inamtazama.
"Ifahamike kuwa utungaji wa Katiba ni zaidi ya vyama vya siasa... hii ni Katiba ya Watanzania wote na kura ya siri itawafanya wajumbe wawe huru kufanya uamuzi kwa masilahi ya umma wa Watanzania," alisema. Bulaya alikosoa mfumo wa kura ya wazi unaotumika katika Bunge la Jamhuri, akisema unamfanya mpigakura kushindwa kutumia utashi wake kufanya uamuzi sahihi akihofu kushughulikiwa na chama chake.

source: Na Daniel Mjema, Mwananchi

Matokeo ya Mtihani wa Kitaifa 2013 Kidato cha Nne na QT

Links za kutizamia matokeo:

  1. Bofya hapa kwa matokeo ya CSEE 2013 
  2. Bofya hapa kwa  matokeo ya QT 2013

source:wavuti.com

Friday, February 7, 2014

Bunge la Katiba Februari 18, majina leo

Rais Jakaya Kikwete akisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam jana.
Rais Jakaya Kikwete jana alitangaza rasmi kuwa Bunge la Katiba litaanza  Februari 18, mwaka huu.
Aidha, alisema kuwa atatangaza majina ya wajumbe wa Bunge hilo leo.

Akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam jana, Rais Jakaya Kikwete alisema maandalizi kwa ajili ya Bunge hilo yanaendelea vizuri na kilichobaki ni marekebisho madogo madogo.

“Wiki iliyopita nilitembelea kwenye ukumbi  wa Bunge la Katiba kwa kweli maandalizi yanaendelea vizuri, viti vimeshafungwa, na vipaza sauti vilikuwa vinafungwa na niliambiwa kuwa mpaka ifikapo Februari 10 (Jumatatu ijayo) kila kitu kitakuwa tayari,” alisema.

Aliongeza kuwa alishauriana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kwamba wamekubaliana kuwa Bunge hilo lianze Februari 18, ingawa sheria inawataka watangaze kuanza kwa kikao hicho cha Bunge hilo siku 21 baada ya kupokea Rasimu ya Katiba na Tangazo hilo bado halijawekwa rasmi, hivyo litatangazwa rasmi Februari 14.

Rais Kikwete aliongeza kuwa Bunge hilo linatarajiwa kuchukua siku 70, lakini lisipomaliza kazi yake kwa muda uliopangwa litaongezewa siku nyingine 20 ili liweze kumaliza kazi yake.

Alisema wananchi walioomba nafasi ya kuwa wajumbe wa baraza hilo ni 3,774 na wanaotakiwa ni 201 na wale walioomba kutoka mashirika mbalimbali ni 1,647 wakati nafasi zilikuwa ni 20.

Aliendelea kufafanua kwamba wajumbe walioomba kutoka Taasisi za Dini walikuwa 329 wakati nafasi zilikuwa ni 20 tu, walioomba kwa kupitia vyama vya siasa walikuwa ni 198 wakati nafasi zilikuwa ni 42, walioomba kutoka Taasisi za Elimu ni 130, huku nafasi zikiwa ni 20.

Walioomba kutoka makundi ya walemavu ni 140 huku nafasi zikiwa ni 20, walioomba kutoka vyama vya wafanyakazi ni 102 wakati nafasi zilikuwa 19, kutoka makundi ya wafugaji 47 wakati nafasi zikiwa ni 10, makundi ya wavuvi ni 57 wakati waliotakiwa ni 10 na makundi ya wakulima ni 157 wakati nafasi zilikuwa ni 20.

“Makundi yenye mrengo unaofanana walikuwa 127 wakati waliochaguliwa ni 10, hivyo watu 3,593 hawatakuwamo ila siyo kwamba hawafai, kwani ukiangalia sifa zao ni wasomi na wana uzoefu,” alisema.

Alisema wengi kati ya watu walioomba walikuwa na sifa na vigezo pamoja na elimu stahiki, lakini ilikuwa ni lazima wapatikane wachache kwa kuzingatia nafasi zilizopo na kwamba wale waliokosa hawakukosa kwa kukosa sifa.

Hata hivyo, Rais Kikwete aliwaasa viongozi na wajumbe wa vyama vya siasa kuweka kando maslahi yao na ya vyama vyao na kuweka maslahi ya Taifa mbele ili kuhakikisha inapatikana Katiba mpya kwa wakati na unaofaa.

Vilevile, alisema bunge hilo ndilo lenye mamlaka ya kupitisha rasimu hiyo na kuwa Katiba, hivyo wajumbe hao wajue wana dhamana kubwa kwa wenzao katika kuipatia nchi katiba nzuri na itakayodumu kwa muda mrefu hata kwa miaka 50 ijayo, ambayo itadumisha Muungano, amani, mshikamano uchumi na maendeleo kwa wananchi.

Rais Kikwete aliwataka wajumbe wa Bunge hilo wajue kinachojadiliwa ni  vile vinavyofaa na visivyofaa, na kwamba vyama vya siasa vina nafasi kubwa sana kwa kuwa Bunge hilo lipo chini ya vyama vya siasa.

“Kufanikiwa kwa Bunge hilo kutatokana na vyama vya siasa, sasa msipoelewana ninyi basi na kule hakuna litakaloeleweka, kufanikiwa kunatokana na ninyi na wanachama wenu, na ndiyo mtakaojenga au kubomoa, mimi nataka mjenge na siyo kubomoa” alisema na kuongeza:

“Tupate Katiba mpya kwa wakati ili ituwezeshe kwenye uchaguzi ujao, mimi naamini vyama vikishirikiana katiba itapatikana bila ya kelele kama vyama vitatambua kuwa tunatengeneza jambo la  wote na siyo la vyama vyao.”

“Hatuendi kule kutengeneza katiba ya CCM, Chadema wala ya NCCR, hilo tukilikamilisha tutakuwa tumevuka kikwazo cha kwanza, kama vyama vitakubali kuongozwa kwa nguvu za hoja watakazotoa wajumbe na siyo nguvu ya hoja ya mjumbe,” alisema Kikwete.

Akisisitiza wajumbe hao kuacha kupinga kila hoja ambayo inatolewa na mtu kwa kuwa tu mtu huyo anatoka chama fulani, na kuunga mkono yale tu yanayotolewa na wajumbe wa chama chake hata kama mtu huyo hana hoja ya msingi.

Aliwataka kuwa tayari kusikiliza maoni ya hata wale wasiowapenda, ili mradi yawe na maana na hoja za msingi kwani ni haki ya kila chama kutoa maoni yao, lakini waende na maoni hayo kama maoni na siyo amri, na hata pale watakapoitana na kuelezana msimamo wa vyama vyao kwa wenzao hilo halina shida.

Aliongeza kuwa ni vyema viongozi wa siasa kwenda kwenye Bunge hilo huku wakiwa na lengo la kuwasikiliza wengine, na mchakato wa katiba hiyo utafanikiwa kwani watu watatofautiana kwa hoja tu na siyo itikadi za vyama vyao.

“Ni vyema tukawa na katiba inayojali maslahi ya Watanzania ndani na nje ya muungano, anakoishi na ndani ya historia yake,” alisisitiza Rais Kikwete.

Aliwaambia viongozi hao wa vyama vya siasa kwama wasipokuwa makini wataivuruga nchi, na kutengeneza lindi la la uadui na kuleta chuki miongoni mwa wananchi.

MUUNGANO, UKOMO UBUNGE
Pia alivitaka vyama hivyo kushirikiana kwenye mijadala migumu zaidi ya mjadala wa mfumo upi ufuatwe kwenye Muungano, ambayo ni ule wa serikali mbili au serikali tatu.

“Kuna mambo magumu kwenye rasimu kwani hata sisi tulipokuwa tunajadili rasimu hiyo tuligundua mambo magumu, kama kile kipengele kinachosema kuwa mtu akiwa ameshakuwa mbunge kwa vipindi vitatu anapoteza sifa za kuwa mbunge,” alisema.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema: “Tanzania ni yetu sote, na ni zaidi ya siasa, hivyo ni vyema tukawa makini katika yale tunayotenda kuliko kusema na kutenda tofauti na tunayosema kwani wananchi wanataka katiba itakayagusa maisha yao.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendelao (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, alisema Rais Kikwete hajagusia jinsi gani watazingatia maoni ya wananchi katika kuijadili rasimu ya katiba hiyo.

Katika mkutano huo viongozi wa vyama vyote 21 vyenye usajili wa kudumu walihudhuria na vingine vilituma wawakilishi wao.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliwakilishwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana; Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula; Dk. Asha-Rose Migiro,  ambaye ni Katibu Siasa na wa Mambo ya Nje na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Vuai Ali Vuai.

Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Dk. Slaa na Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu ya chama hicho, Victor Kimesera.

Pia alikuwapo Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, Mwenyekiti wa Chausta, James Mapalala na Peter Kuga Mzirai ambaye ndiyo Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Bunge hilo linaundwa na wajumbe 635 ambao ni 358 kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wajumbe 76 kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na wajumbe 201 kutoka mashirika yasiyo ya serikali pamoja na taasisi za kidini.
 
CHANZO: NIPASHE

Tuesday, February 4, 2014

JB, Uwoya wajiunga CCM

wasanii1 772ce

STAA wa Bongo Movie, Jacob Stephen maarufu kama JB ameongoza wasanii wengine tisa kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya chama hicho zilizofanyika jijini Mbeya juzi Jumapili. (HM)
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliwatambulisha wasanii hao ambao baadhi yao walikuwa wamevaa sare za kijani zinazotumiwa na chama hicho, huku akieleza kuwa wamejiunga CCM baada ya kutambua ubora wa chama hicho.
Kwenye orodha hiyo, wasanii wa filamu walioungana na JB kuwa wanachama wa CCM ni pamoja na Irene Uwoya, Single
Mtambalike 'Richie', Blandina Chagula 'Johari', Tamrina Poshi 'Amanda', Haji Adam 'Baba Haji', Slim Omari, Salum Haji 'Mboto' na Wastara wakati msanii wa muziki ni Banana Zorro.
"Kabla ya kuanza kwa sherehe yetu napenda kuwatambulisha wasanii wa filamu na muziki ambao wameamua kujiunga na CCM leo (jana Jumapili), watakabidhiwa kadi zao baadaye na Mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete," alisema Nape.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake JB alisema: "Naomba mashabiki wetu wote ambao hawana mapenzi na
CCM watusamehe sana kwa uamuzi wetu wa kujiunga na chama hiki. Tumeona ndiyo sehemu nzuri na tumeamua kujiunga rasmi."
Naye Wastara alisema: "Tumezaliwa ndani ya CCM, tumekulia CCM na tunaendelea kuishi ndani ya CCM."
Baadhi ya wasanii wengine waliojitosa kwenye siasa ni pamoja na Joseph Haule maarufu kama Profesa J, Seleman Msindi 'Afande Sele' na Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, ambaye Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chadema. 

Chanzo: mwanaspoti

Utafiti: Ngono ya mdomo ni hatari

kansa1 74ce1
Leo ni siku ya Saratani Duniani. Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini idadi ya vijana ambao ni tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana kuangamia kwa saratani ikiwemo ya koo. (HM)
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama 'Oral Sex".
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.
Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya koo ni ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi (Karposi's Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
"Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa," anasema Dk Kahesa na kuongeza.
"Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,"anaongeza
Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini saratani ya koo inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea hiyo inaonyesha kuwa wengi wao walianza ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa bado wadogo.
"Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao," anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya kwanza ni "Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote hutofautiana wakati zinapimwa kwenye darubini lakini
Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona viashiria kwani mwanzo mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari wamechelewa kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.
"Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri siku zinavyokwenda ndiyo kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi mmoja," anasema.
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi hospitali ili aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa kugundulika na kuanza matibabu.
Kama saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo vyote vilivyopo jirani na koo na hadi kufika katika tezi au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa maalumu ambacho ni kemikali.
Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992 kulikuwa na kati ya watu 546 waliopimwa, wanaume 430 na wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Utafiti huo ulishirikisha watu wenye umri wa miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa miaka 50-59 tofauti na hali iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri vijana wenye umri wa miaka 40.
Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka saba iliyopita takwimu za taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167 hadi kufikia wagojwa 277. Hali inaonekana huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi wa watu wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia midomo.
Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi.
Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana na kiungo chenye athari hizo.
Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati ya magonjwa ya zinaa ambao huambukizwa kwa bakteria na kwamba ugonjwa huu pia huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalili kwa muda mrefu.
Hepatitis A: Hiki ni ni kirusi kinachopatikana katika kinyesi cha binadamu, kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda kunyonya na kulambana sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika macho hadi kupofuka.
Hepatitis B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi vya Ukimwi kwa sababu virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za siri na damu. Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na vipele vingi na hata majipu ambayo huwa magumu kupona na wapo wanaokufa.
Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C: ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu
inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa kunyonyana sehemu za siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi vya Ukimwi kwa uchache lakini kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya kondom ambazo huvaliwa katika mdomo wa binadamu na hivyo kupunguza hatari ya kupata madhara hayo.
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema hakuna utafiti wa moja kwa moja unao onyesha kuwa baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume.
"Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume wanafanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo hilo lipo licha ya kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume hawana nguvu za kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya nao mapenzi kwa njia yam domo"anasema.
NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na saikolojia wanasema kuna njia nyingi za kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za siri.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake na kwamba staili hizo ni staili za wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi ya utandawazi.
Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu huiga staili hizo kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna zina madhara makubwa, hivyo ni jukumu la kila mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii kina manufaa la hashaa! vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha. 

Chanzo: mwananchi

Monday, February 3, 2014

Ivo Mapunda mkali balaa!

ivoclip 66ab9

KIPA wa Simba, Ivo Mapunda amesisitiza ataendeleza ukali wake kwa wachezaji wote wa Simba anapokuwa uwanjani ili wazidi kuwa makini kiuchezaji. (HM)
Mapunda alisema: "Mimi huwa nina mikakati ninapokuwa uwanjani, nataka kuona wachezaji wenzangu wakiwa makini na kuendana na jinsi mpira unavyochezwa.
"Saa nyingine wanajisahau na ni haki yangu kuwakumbusha ingawa wanatafsiri kuwa mimi ni mkali lakini ina faida kwani mwishowe timu inapofungwa anayekuwa wa mwisho golini ni mimi," alisema.
"Huwa nakua mkali kwa mabeki wangu nikitaka wawe makini zaidi kwenye mpira, pia wakati mwingine mazingira yakiwa magumu huwa nawakumbusha viungo na washambuliaji kuwa makini kwani wanaiweka timu hatarini kwa kiasi fulani wasipokuwa makini.
"Unajua mimi sipendi kufungwa mbali na timu yangu kupoteza mchezo, naamini kama kina Donald (Mosoti), Owino (Joseph), Kaze (Gilbert) na mabeki wengine wanakuwa makini basi kila mchezaji ataonekana bora na timu pia itaonekana bora."
Mara kwa mara Mapunda amekuwa akiwakaripia wachezaji wenzake hususan wale wa nafasi za beki na kiungo huku wakati mwingine akiwasukuma akiwataka wakakabe hususan katika mipira ya kona na adhabu. 

Chanzo: mwanaspoti