
Makadinali 19 wepya wa Kanisa Katoliki
wametawazwa leo katika sherehe iliyofanywa Vatikani - uteuzi wa kwanza
kufanywa na Papa Francis tangu kuchukua uongozi wa Kanisa Katoliki.
Ameteua viongozi wa kanisa kutoka nchi 12 zikiwemo Haiti, Burkina Faso na Ivory Coast ambao walivishwa majoho na kofia nyekundu.
Papa mstaafu, Benedict wa kumi na sita, naye alihudhuria, akionekana kwenye ibada ya hadhara kwa mara ya kwanza tangu kustaafu.
Mwandishi wa BBC Vatikani anasema
uteuzi wa makadinali aliofanya Papa Francis unaonesha amebadilisha dira
kutoka Ulaya na kuelekea maeneo ambako Kanisa Katoliki lina nguvu, yaani
Amerika Kusini na Kati na Afrika.
Na kadinali mwengine mpya ni mkuu wa Kanisa Katoliki la Uingereza naWales, Askofu Vincent Nichol.
Chanzo, bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment