Leo ni siku ya Saratani Duniani.
Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini idadi ya vijana ambao ni
tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana kuangamia kwa saratani
ikiwemo ya koo. (HM)
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya
Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo
husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama 'Oral Sex".
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti huo wa hivi karibuni,
ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa
na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444
wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia
kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya
kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi
wao katika kushiriki ngono.
Vijana wenye umri huo ndio wahanga
wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi,
huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni
wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima
walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo
kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia
hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani
kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema
saratani ya koo ni ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata
wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi (Karposi's Sarcoma) ambayo
huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24
zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna
baadhi ya watu hupata saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao
na wengine kuwa na umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo,
lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
"Hali hii ya vijana wenye umri huo
kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao,
lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume
ili aweze kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini
zamani staili hii haikuwepo kabisa," anasema Dk Kahesa na kuongeza.
"Kuna njia nyingi tu za kumvutia
mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi
nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna
njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa
mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo
hicho,"anaongeza
Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo
imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia
muda mwingi kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu
wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya
wagonjwa wote wa saratani nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo
kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo
ya wenzetu wazungu ambayo mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema katika mtiririko wa saratani
zinazoongoza nchini saratani ya koo inashika nafasi ya tano, wagonjwa
wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na
kuendelea hiyo inaonyesha kuwa wengi wao walianza ngono ya mdomo muda
mrefu wakati wakiwa bado wadogo.
"Asilimia kubwa ya wagonjwa
wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu wenye umri wa
kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao kuanza mapema
vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au wengine
kurithi kutoka kwa wazazi wao," anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za
saratani ya koo; aina ya kwanza ni "Oesophagus Carcinoma na Squamous
cell carcinoma, zote hutofautiana wakati zinapimwa kwenye darubini
lakini
Dalili za saratani ya koo
Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za mgonjwa wa
saratani ni chakula kukwama kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza
kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa
kumeza hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu
kugundua na kuona viashiria kwani mwanzo mgonjwa huanza kupata shida
kumeza chakula na kwamba wagonjwa wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya
Saratani wanakuwa tayari wamechelewa kwani wanakuwa katika hatua ya
mwisho.
"Unaweza usionyeshe dalili lakini
kadri siku zinavyokwenda ndiyo kunakuwa na dalili zinajitokeza pia
katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu wakati wa kumeza chakula,
maumivu katika kifua na mgongo na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi
kikavu kinachoweza kudumu mwezi mmoja," anasema.
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa
kuhawi hospitali ili aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba
mgonjwa anayewahi kupata matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule
ambaye amechelewa kugundulika na kuanza matibabu.
Kama saratani hiyo itakuwa
imeshambulia viungo vyote vilivyopo jirani na koo na hadi kufika katika
tezi au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa kwa njia ya
upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa maalumu ambacho ni kemikali.
Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya
tafiti zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema kuwa kati ya mwaka 1983
hadi 1992 kulikuwa na kati ya watu 546 waliopimwa, wanaume 430 na
wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Utafiti huo ulishirikisha watu wenye
umri wa miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye
umri wa miaka 50-59 tofauti na hali iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo
unawaathiri vijana wenye umri wa miaka 40.
Dk Kahesa anasema katika kipindi cha
miaka saba iliyopita takwimu za taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka
wagonjwa 167 hadi kufikia wagojwa 277. Hali inaonekana huenda
ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi wa watu wanaonekana
kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia midomo.
Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza
kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na
gonjwa wa gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni
huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila
baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi.
Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao
huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo
unapokutana na kiungo chenye athari hizo.
Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja
wapo kati ya magonjwa ya zinaa ambao huambukizwa kwa bakteria na kwamba
ugonjwa huu pia huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza
wasijijue maana huwa hauna dalili kwa muda mrefu.
Hepatitis A: Hiki ni ni kirusi
kinachopatikana katika kinyesi cha binadamu, kirusi hiki huwaingia wale
wanaopenda kunyonya na kulambana sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa
ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika macho hadi kupofuka.
Hepatitis B: Ugonjwa huu huambukizwa
kama virusi vya Ukimwi kwa sababu virusi vyake hukaa katika majimaji
yanayotoka katika sehemu za siri na damu. Mtu akiwa na ugonjwa huu,
mwili wake unakuwa na vipele vingi na hata majipu ambayo huwa magumu
kupona na wapo wanaokufa.
Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C: ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu
inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana
raha kwa kunyonyana sehemu za siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz
ya virusi vya Ukimwi kwa uchache lakini kwa nchi zilizoendelea wamebuni
aina ya kondom ambazo huvaliwa katika mdomo wa binadamu na hivyo
kupunguza hatari ya kupata madhara hayo.
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema hakuna utafiti wa
moja kwa moja unao onyesha kuwa baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa
njia ya mdomo wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume.
"Utafiti wa mtu mmoja hautoshi
kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume wanafanya ngono kwa njia ya mdomo
wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo kinachotakiwa ni kufanya
utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo hilo lipo licha ya kuwepo kwa
kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume hawana nguvu za kiume na
wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya nao mapenzi kwa njia yam
domo"anasema.
NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na
saikolojia wanasema kuna njia nyingi za kuandaana wakati wa tendo la
ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za siri.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa
mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake na kwamba staili
hizo ni staili za wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa
kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi
kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi ya utandawazi.
Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi
ya watu huiga staili hizo kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna
zina madhara makubwa, hivyo ni jukumu la kila mtu kulinda afya yake na
ya mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika
mitandao ya kijamii kina manufaa la hashaa! vitu vingine vinachangia
kuhatarisha maisha.
Chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment