Tuesday, July 23, 2013

MIILI YA WANAJESHI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA YAWASILI KIWANJA CHA NDEGE CHA ZANZIBAR


  Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza la Koplo Mohamed Juma Ali aliyeuawa Daafur katika harakati za kulinda amani chini ya Kikosi cha  Umoja wa Mataifa (Unamid) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Zanzibar Jana.
  Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza la Sajent Shaibu Shehe Othman aliyeuawa Daafur katika harakati za kulinda amani chini ya Kikosi cha  Umoja wa Mataifa (Unamid) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Zanzibar  jana.
 Baadhi ya Wanajeshi wakiwa wamebeba Majeneza ya Maiti za Marehemu Sajent Shaibu Shehe Othman na Koplo Mohamed Juma Ali waliofariki Daafur katika harakati za kulinda amani chini ya Kikosi cha  Umoja wa Mataifa, mara baada ya kuwasili kiwanja cha ndege cha Zanzibar jana .
Mke wa marehem Sajent Shaibu Shehe Othman mwenye Juba jeusi akiwa ameshikiliwa na ndugu na Askari kutokana huzuni alokuwa nayo mara baada ya kuwasili mwili wa Mume wake.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
---
Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliouawa Darfur wiki iliyopita  Sajent Shaibu Shehe Othuman wa Mpendae na Koplo Mohamed Juma Ali wa Kwarara imekabidhiwa jana kwa familia zao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar.

Marehemu hao wawili wenye Asili ya Zanzibar ni miongoni mwa Askari saba wa JWTZ waliuawa walipokuwa wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa na Afrika UNAMID,huko Darfur. Miili ya marehemu hao imewasili majira ya saa 9 alasiri kwa ndege ya JW 90 34 aina ya Boing ikitokea katika Hospitali ya JWTZ Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kuwasili Uwanjani hapo Miili ya Marehem hao ilipokelewa na Katibu mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Khalid Mohamed Salum akifuatana na Mwenyeji wake Bregedia Jeneral Kamanda wa Bregedi ya Nyuki Sharif Sheikh Othuman Viongozi wa Vyama na Serikali,Wanafamilia pamoja na Wananchi kwa ujumla. Aidha huzuni ziliendelea kutanda kwa ndugu na Jamaa waliofika kupokea maiti hizo za 

Wapiganaji wa Amani ya Dunia chini ya mwamvuli wa UNAMID. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shughuli za Mazishi zitafanyika kesho saa nne za asubuhi  katika makaburi ya Mwanakwerekwe nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Aidha shughuli hiyo ya Mazishi itaambatana na taratibu za kijeshi zitakazofanyika Makaburini hapo.
 
source: haki ngowi

Sunday, July 21, 2013

Ni Vilio ...vilio

Ni baada ya miili saba ya wanajeshi waliouawa Darfur kuwasili Dar
Kuagwa kesho...kila mpiganaji aliyeuawa atafidiwa sh. milioni 113

 
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba moja ya majeneza saba yaliyobeba miili ya wanajeshi waliokuwa katika kikosi cha Umoja wa 
 
Mataifa cha walinda amani wa Darfur nchini Sudan.
Vilio na mayowe jana vilitawala Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere jijini, Dar es Salaam, wakati miili ya askari saba wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ilipowasili kutoka Dafur nchini Sudan.

Askari hao waliuawa Jumamosi iliyopita kwenye shambulizi la kushtukiza, huku wengine kujeruhiwa.
Ndugu wa marehemu wakiwemo watoto, wake zao na marafiki walikuwa wakilia wakati wote tangu miili hiyo ilipowasili uwanjani hapo na kushukia Terminal 1-Air wing (kikosi cha anga).

Baadhi ya jamaa za marehemu walishindwa kuzungumza , wengine wakishikiliwa kuwazuia wasianguke kutokana na huzuni ya msiba huo.
Ndege maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) yenye namba B 737- 400 COMBI, ilileta miili hiyo na kutua uwanjani hapo saa 10:45 jioni.

Miili hiyo iliondolewa na kuingizwa katika magari  saba ya JWTZ kila mmoja ukisafirishwa peke yake kwenye msafara ulioongozwa na pikipiki za jeshi na kupelekwa Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, aliwaongoza viongozi wa serikali akiwamo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, pamoja na mamia ya wananchi waliofika uwanjani kuwapokea marehemu hao.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja, alisema marehemu wataagwa kesho saa 2:30 asubuhi katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga jijini.

Alisema miili hiyo itaagwa kwa heshima zote za kijeshi na baadaye kusafirishwa kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza uwanjani hapo, msemaji wa familia ya Sajenti Shaibu Othumani, alisema wamepata pigo kubwa kwa kuwa ndugu yao alikuwa tegemeo katika familia hiyo.

Shemeji wa marehemu Othuman aliyejitaja kwa jina la Rehema akizungumza huku akiwa analia alisema wamepatwa na majonzi na kwamba ni vigumu kumsahau mtu waliyetoka naye mbali.

Wanajeshi hao ni Sajenti Othuman , makoplo Oswalid Chacha, Mohamed Juma na Mohamed Chukilizo. Wengine ni maprivate Rodney Ndunguru , Peter Werema na Fortunatus Msoffe.

FIDIA KWA MAREHEMU
Kila mpiganaji aliyeuawa atafidiwa Dola za Marekani 70,000 ( karibu Sh. milioni 113) kwa mujibu wa viwango vya Umoja wa Mataifa (UN).

Fedha hizo zimetajwa na vyombo vya habari vya kigeni kuwa ni kiwango kinachotolewa na UN kwa askari anayeuawa akiwa kwenye operesheni za kulinda amani zinazosimamiwa na chombo hicho.

Wapiganaji saba kati ya 14 wa JWTZ walioko Dafur kwenye kikosi cha kulinda amani kinachoundwa na UN pamoja na Umoja wa Afrika (Unamid), Jumamosi iliyopita waliuawa baada ya kushambuliwa kwenye tukio la kushtukiza.

Chini ya utaratibu wa UN wa fidia, kila mpiganaji aliyepoteza maisha atafidiwa Dola 70,000 kwa mujibu wa taarifa za Radio Sauti ya Ujerumani (DW) Idhaa ya Kiswahili, zilizotangazwa jana asubuhi.

DW ilifanya mahojiano na Kaimu Msemaji wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya JW, Meja Joseph Masanja na kumhoji kuhusu fidia hiyo kutolewa kwa jamaa waliopoteza ndugu zao .

Akijibu Kaimu Msemaji wa JW alisisitiza kuwa fidia ya marehemu hao itakuwepo lakini hakupinga kiwango cha (UN) wala kukubali badala yake alisema kinachofanyika kwa wakati huu ni kuwaleta marehemu hao nchini na kuwafikisha sehemu ambazo jamaa zao wamezitayarisha kwa ajili ya kuwazika.

Kama familia hizo zitafidiwa kiasi hicho, kila aliyepoteza jamaa yake atapokea zaidi ya Sh milioni 100 bila kuhusisha fidia kwa taifa. (Dola ni karibu Sh 1,620).

Katika mahojiano hayo, Kaimu Msemaji wa JWTZ aliulizwa iwapo serikali ina mpango wa kuwafidia askari hao, hata hivyo alikwepa kujibu swali hilo na kuzungumzia zaidi juu ya kuwapokea na kuwazika.
 
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Thursday, July 11, 2013

OBAMA OBAMA


NIMEIPENDA HII

Picture

Aliyeruhusu masanduku ya Agnes na Melisa yapite na dawa za kulevya JNIA... (?)

Polisi imekiri kuwa wasichana wawili raia wa Tanzania waliokamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Sh. bilioni 6.8, walipitia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Wasichana hao walisafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la South African Airways linalomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema hayo jana wakati akizungumza katika mahojiano na NIPASHE iliyotaka kujua kama wasichana hao walipitia uwanja gani na kama walikaguliwa na maofisa wa uwanja huo.

“Kila mtu anapopita uwanja wa ndege anakaguliwa na kama ana kitu ambacho ni kibaya ndipo anakamatwa, hawa wasichana walikaguliwa maana huwezi kupita uwanja wa ndege bila kukaguliwa,” alisema Kamanda Nzoa.

Kamanda Nzoa alisema si jukumu la Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi kwenye viwanja vya ndege, lakini ni 
jambo la kawaida mtu kukamatwa nchi nyingine na dawa za kulevya wakati katika nchi aliyoanzia safari hajakamatwa kwani inategemea utalaamu wa watu wenyewe wanaokagua.

Alisema kinachotakiwa watu wa uwanja wa ndege ni lazima wawe na mtu au wakaguzi ambaye ni mtaalamu sana wa kutambua dawa za kulevya kwa kuwa ziko za aina nyingi na mbinu nyingi zinatumika kuzisafirisha.
Aidha, alisema dawa za kulevya ni nyingi na siyo cocaine tu ambayo imezoeleka mara kwa mara.

“Utakumbuka Juni 23 mwaka 2010 nilikamata mabalozi wawili, hawa watu walitoka Brazil wakaenda Afrika Kusini, lakini tukawakamatia hapa Tanzania,” alisema Nzoa.

Aliongeza kuwa hivi sasa wasichana  hao wamekwisha kufunguliwa mashtaka nchini Afrika Kusini.

Kamanda Nzoa alisema uchunguzi unaendelea kumbaini mmiliki wa dawa hizo na kuna dalili za kuwabaini wahusika hao.

Dawa hizo zilisafirishwa kama mizigo mingine inayokaa sehemu za mizigo ndani  ya ndege kwani uzoefu unaonyesha kwamba kwa namna yoyote ile abiria hawezi kuruhusiwa kwenda  kukaa na mzigo wake ndani ya ndege unaofikia kilo 150.

Uzoefu unaonyesha kwamba kwa kawaida ndege kulingana na ukubwa wake zimekuwa zikiruhusu abiria kupanda na kukaa na mizigo yao ya mkononi isiyo na uzito mkubwa.

Baadhi ya ndege zinaruhusu abiria kupanda ndani ya ndege wakiwa na mizigo yao ya mkononi isiyozidi uzito wa kilo kumi wakati mzigo unaokaa kwenye mizigo chini baadhi ya mashirika ya ndege huruhusu uzito wa kuanzia kilo 20 hadi 40.

Katika hali ya kawaida, hata kama wasichana hao wangeamua kugawana dawa hizo kwa usawa, kila mmoja angebeba kilo 75, kiasi ambacho hata hivyo abiria haruhusiwi kupanda nacho kama mzigo wa mkononi, wala mzigo ambao haulipiwi.

Kwa hali hiyo, mizigo hiyo ililipiwa gharama za ziada za usafirishaji kwa kuwa hakuna shirika la ndege lenye unafuu wa mizigo ya bure kwa abiria wake kwa uzito wa kilo 75.

Jitihada zinaendelea kumtafuta Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), kujua ilikuwa je watumishi waliokuwa zamu siku ambayo mzigo huo ulisafirishwa kuelekea nchini Afrika Kusini hawakutambua dawa hizo.

--- Imeandiwa na THOBIAS MWANAKATWE via gazeti la NIPASHE

Thursday, July 4, 2013

TUJIKUMBUSHE MATUKIO MBALIMBALI ZIARA YA OBAMA TANZANIA

     Rais Barack Obama alivyowasili Tanzania

 Maofisa Usalama wa Marekani, wakiingia Uwanja wa Ndgege wa Zamani, jijini Dar es Salaam, ilikotua ndege ya Rais Barrack Obama wa Marekani  kwa ajili ya kuimarisha ulinzi uwanjani hapo jana.


Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, ni miongoni mwa Viongozi waliofika kumpokea Rais wa Marekani Barack Obama, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Tanzania. 
Ndege iliomchukuwa Rais Obama ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere

Ndege ya Rais wa Marekani, Barrack Obama, 'Airforce One' ikiwa imetua tayari, uwajani hapo.
 
 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Balozi Alfonso, wakiende kumpokea Mgeni wao Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili katika Uwanja wa Mwalim  Nyerere kwa ziara ya Siku mbili kutembelea Tanzania akitokea Nchini Afrika ya Kusini. 
Rais wa Marekani akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere kwa ziara ya siku mbili, akiongozana na Mkewe na Watoto wake wakishuka katika ndege yake.  
Rais Obama akiteta na Mwenyeji wake Rais Kikwete alipowasili Tanzania akiwa katika ziara ya siku mbili Tanzania.
Rais Obama akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakielekea katika jukwaa maalum aliloandaliwa kwa ajili ya kupingwa wimbo wa Mataifa haya mawili  
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Marekani Barack Obama. wakiwa katika uwanja wa ndege.

 

8E9U8352

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Marekani Barack Obama wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar leo
8E9U8357
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete akimtambulisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa Rais wa Marekani Barack Obama
8E9U8374
Makamu wa pili wa Rais , Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Rais wa Marekani Barack Obama wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar leo
8E9U8382
Spika wa Baraza la wawakilishi , Zanzibar Pandu Ameir Kificho akisalimiana na Rais wa Marekani Barack Obama wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar leo

 

 
 










Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Marekani Barack Obama, katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam jana, akiwa nchini katika  ziara ya siku mbili kwa mualiko wa kiserikali.

 alipowasili Uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea mgeni wake, Rais wa Marekani, Barrack Obama.


 

Rais Barraka Obama akishuka na mtoto wake mkubwa Mallya, uwanjani hapo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku mbili nchini.


Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama, Michelle Obama, akishuka kwenye ndege hiyo na mtoto wake, Sasha.


Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama 'First lady' akikumbatiana na Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo na mumewe (kulia), leo mchana.


 Rais Obama akipokea maua kutoka kwa mtoto Zakia Minja, uwanjani hapo.


Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili uwanjani hapo jana mchana.


Rais Obama akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21.


Rais Obama akitoka kukagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21, uwanjani hapo jana.


Rais Barrack Obama akiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima uwanjani hapo, mara baada ya kuwasili jana mchana.


Rais Barrack Obama akisalimiana na mke wa Rais Kikwete, Mama Salama mara baada ya kupokea gwaride la heshima uwanjani hapo.


 Rais Barrack Obama, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.


 Akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.


 Hapa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.


 Akisalimiana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.


Hapa Rais Obama na mwenyeji wake, Rais Kikwete, wakifurahia ngoma ya Mganda ya asili ya Wangoni, mkoani Songea.


Hapa Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuondoka Uwanja wa ndege.


Wananchi wakiwa wamekusanyika nje ya jengo la Ikulu kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama.


Wananchi waliokusanyika nje ya jengo la Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama,wakipunga bendera za Tanzania na Marekani. 





Maofisa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwa nje ya Ikulu, kumkaribisha Rais, Barrack Obama.


Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma (kulia), akiwa na mgeni wake, First lady, Michelle Obama, kwenye Ofisi za Wama.


Hapa wakiwa Makumbusho ya Taifa, wakipokea mau kwa ajili ya kuweka kwenye mabaki ya vifaa vilivyolipuliwa na bomu kwenye Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam.


Wake hao wa Marais wa Marekani na Tanzania, wakiweka mashada hayo kwenye mabaki hayo kwa ajili ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao kwenye tukio hilo.


Wakiwaombea wahanga hao, mara baada ya kuweka mashada hayo ya maua.


Rais Obama Akionyesha Shoo ya Kabumbu Ubungo

Rais  Jakaya Kikwete  wa  Tanzania  akimpasia mpira  Rais  Barack Obama wa Marekani  leo kama  sehemu ya kuonyesha  uwezo  wao  kisoka pia

Hapa  Rais  Obama  akionyesha  ujuzi  katika  soka eneo la Ubungo




Rais Jakaya  Kikwete  kulia akimtazama  Rais wa Marekani Barack Obama akionyesha uwezo  wake katika  soka eneo la Ubungo  leo
Mbali ya  kuwa Rais wa dunia  pia katika  soka yumo  Rais Obama 


  Rais Obama na  Kikwete watembelea mradi wa Umeme wa Symbion Ubungo

8E9U0188 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mwenyeji wake Rais Barrack Obama wa Marekani wakipata maelezo juu ya kituo cha uzalishaji wa Umeme Ubungo kinachoendeshwa na kampuni ya symbion power wakati viongozi hao walipofanya ziara katika kituo hicho leo asubuhi.Watatu kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Symbion Power Bwana Paul Hinks(picha na Freddy Maro) 8E9U9730 8E9U0198

Serikali ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan chi hizo.

Kauli hiyo ilitolewa jana  mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.

Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.

 “Sasa ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani  ili kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema Rais Obama.


Aliongeza kuwa pia ushirikiano huo unapaswa kuboresha utoaji wa mizigo katika bandari ya Dar  es salaam na Mombasa  kwenda nchi zisizo na bandari ili kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini.

Akizungumzia hotuba ya Rais Obama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini (CTI) Felix Mosha alipongeza hotuba hiyo kwa kufungua ukurasa mpya kwa nchi za Afrika na Marekani kwa kuonyesha kuwa wakati wa kutegemea misaada umepitwa na wakati badala yake ni kushirikiana katika uwekezaji.
Katika mkutano huo kiasi cha wafanyabiashara 170 walihudhuria mkutano huo

picha na habari kwa hisani ya Zenjinews; Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com na Francis Godwin Mzee wa matukio