Wednesday, June 26, 2013

MZEE VIPI WATU WASEMAJE?

 Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu,  Mizengo  Pinda baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma juni 25, 2013 kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM na Baraza  la Mawaziri.Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma juni 25, 20913  kwa ajili ya kuongoza kikao cha kamati Kuu ya CCM na Baraza la Mawaziri. 
Picha na Ofisi ya waziri Mkuu

Tuesday, June 18, 2013

HII IMEKAAJE?

Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akijadiliana jambo na Mke wa hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere
 
SOURCE: Haki Ngowi

Wednesday, June 12, 2013

MHESHIMIWA MIZENGO PINDA



 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge waBunda na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Utatibu, Mhe. Stephen Wasira. Bngeni Mjini Dodoma Juni 12, 2013.
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Bungeni mjini Dodoma Juni 12, 2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
SOURCE: HAKI NGOWI

upigaji wa picha za utupu

 WP Amisa
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imemfukuza kazi askari wake wa kike, WP Amisa, aliyekuwa akifanya kazi kituo cha Polisi Magomeni kutokana na utovu wa nidhamu.

 Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Suleiman Kova amesema, Amisa amefukuzwa kazi kwa kuwa amekiuka maadili ya Jeshi kwa kitendo chake cha kupiga picha za utupu zilizoonekana katika mitandao.

Amesema, baada ya uchunguzi wa muda mrefu hasa baada ya taarifa na malalamiko ya watu kuhusu askari huyo, Juni 7 Jeshi hilo lilimtia hatiani askari huyo baada ya kujiridhisha na mwenendo mzima wa picha katika mitandao hiyo.
 
source: Haki Ngowi

RASIMU YA KATIBA





Picture

Friday, June 7, 2013

Mazishi ya Mwanamuziki Mashuhuri Nchini Albert Mangwea Mjini Morogoro

 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mangwea
Mwili wa Msanii mashuhuri Alber Mangwea ukiwasili
  Mbunge wa Mbeya, mjini-Chadema Joseph Mbilinyi akitoa heshima za mwisho.
Rafiki wa Karibu wa Marehmu Mangwea M 2 The P akilia kwa uchungu wakati akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu albert mangwea
 Waombolezaji wakishusha jeneza lililokuwa na mwili wa msanii mahiri wa Hip Hop, marehemu Albert Mangwea, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika mjini Morogoro jana
  Jeneza likishushwa kaburini.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akimfariji mama mzazi wa marehemu, Albert Mangwea.
Umati wa watu wakiwa nje ya Uwanja wa Jamhuri wakati wa kutoa heshima za mwisho.Picha Zote na Dande Francis
 
source: haki ngowi

Thursday, June 6, 2013

MALKIA WA TAARAB HADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE LEO

 
Jafari Ally(Kulia) enzi za uhai wake akiwa na mkewe Malkia wa Mipasho nchini Tanzania, Khadija Omar Kopa wakifuatilia semina ya kilimanjaro Kili Awards 2012

Habari zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Kijana mtanashati aliyekuwa Mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, aliyefahamika kwa jina la Jafari Ally, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akitibia kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na kifua.

Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008. Wakati kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini. 

Ratiba kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa huenda msiba huo ukawa  maeneo ya Chaline au Lugoba ambako ni nyumbani kwa wazazi wa Marehemu.
 
SOURCE: HAKI NGOWI

KOVA OYEEE

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP) Suleiman Kova akijipongeza baada ya kuvishwa cheo hicho cha Kamishna wa Polisi (CP) na Mkuu wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi al Polisi