Friday, April 10, 2015

MGOMO WA MADEREVA WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI WATIKISA NCHI LEO

hare on google_plusone_shareShare on twitter

Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.
Wakina MAMA hawa wakiwa wamemshikilia Mgonjwa wao waliekuwa wakimsafirisha kwente mkoani, wakiondoka stendi ya kuu ya Mabasi Ubungo baada kukosa usafiri kutokana na mgomo wa vyombo hiyo leo.
Huku Ubungo mambo yako namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.
Mijadala ikiendelea kwa wadau mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar.
Mara lori likazuiliwa na watu hawa, wakidai kuwa amepakia abiria hivyo anatakuwa kuwashusha KAMAanataka kuendelea na safari yake.
Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama barabarani.
Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna BASIhata moja lililoondoka huku daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.
Uongozi wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni, kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.(Muro)
source: Mjengwa blog

Thursday, April 2, 2015

ASKARI WALIOUAWA, KUPORWA SILAHA PWANI WAAGWA DAR

Mwili wa SCT Francis ukiingizwa katika bwalo la polisi Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuagwa.
Mwili wa CPL Michael nao ukipelekwa kwa ajili ya kuagwa.

Mke wa marehemu Michael (katikati) akilia kwa uchungu.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova akiteta jambo na MC wa shughuli huyo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecki Sadick, akimkaribisha Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu.
IGP Mangu akitoa salam za rambirambi.
…Akipita kuaga miili ya marehemu.
Kamanda Kova akipita kuaga miili ya marehemu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akisalimiana na mke wa marehemu Michael. ASKARI wawili wa jeshi la polisi waliouwawa na kuporwa bunduki aina ya SMG huko Mkuranga mkoani Pwani wameangwa leo katika ofisi za polisi zilizoko Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)
 
source: matukio na vijana