Friday, March 29, 2013

Taswira:Huzuni Yatawala Kifo Cha Mbunge wa Chambani(CUF),Marehemu Salim Hemedi Khamis Spika Wa Bunge Anne Makinda Aifariji Familia




 Spika wa Bunge, Anne Makinda,akimfariji Mke wa Marehemu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge, Anne Makinda akimpa pole, Asla Saidi Zaharani ambaye ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Chambani, Marehemu Salim Hemedi Khamis  aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
  Mke wa Mbunge wa Chambani Marehemu Salim Hemedi Khamisi wa pili kulia, Asla Saidi Zaharani, akili kwa uchungu baada ya kupewa taalifa ya kifo cha mume wake.
   Baadhi ya watoto wa Marehemu, Salim Hemedi Khamisi wakiwa na hudhuni kutokana na kifo cha baba yao mpendwa.
  Spika wa Bunge, Anne Makinda, akiwafaliji viongozi wa Chama cha wananchi CUF kutokana na kifo cha mbunge wao,Salim Hemedi Khamisi,Salim Hemedi Khamisi, katika Hosptali ya Taifa Muhimbili
   Waziri wa Ulinzi, Shamshi Vuai Nahodha,akisalimiana na wanafamilia wa marehamu, Salim Hemedi Khamis
 Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Wananchi CUF wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakijadilijambo wakati wakisubili mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamisi, Mbunge wa Chambani Pemba, Dar es Salaam.Baadhi ya familia ya Mbunge wa Chambani Marehemu, Salim Hemedi Khamisi, wakiwa na hudhuni kumwa baada ya mpendwa wao kufaliki dunia.Picha Zote na Mdau Dande Francis naSalhim Shao

 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa na Mbunge wa Mafia Mhe Abdulkarim Shah alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika Anne Makinda alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
Rais jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 na kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa wafiwa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 alipoongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
Kaimu Katibu wa Bunge Mhe John Joel akisoma wasifu wa marehemu
Rais jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongzi wa kitaifa na wabunge katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambako aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
Wabunge wanawake wakiwa katika maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.Picha na IKULU

NENO FUPI LA USIKU HUU: MTOTO AKIKUMWAGIA BAKULI LA MAJI MACHAFU...!


c1 00aed


Ndugu zangu,


Fikiri mtu mzima unajipitia na hamsini zako ukiwa umevalia nadhifu. Ghafla anatokea mtoto wa miaka sita anakumwagia bakuli la maji machafu. Unafanyaje?


Naam, hapo ndipo mwanadamu unatakiwa utangulize hekima na busara. Maana, kwa kawaida, katika hali kama hiyo, kwa hasira utamzabua kibao huyo mtoto.


Hapana, hupaswi kufanya hivyo hata kidogo. Unapaswa utulie kwanza kama mtu aliyemeza vipande vya barafu. Tafakari kwa kina. Utambue kuwa si bure. Huyo mtoto kuna aliyemtuma, tena si mtoto mwenziwe, bali mtu mzima kama wewe.


Na uione afadhali ya kumwagiwa bakuli la maji machafu kuliko ndoo ya matope. Jiendee zako taratibu. Na ukiweza, si vibaya ukampa pole huyo mtoto aliyekumwagia maji machafu, badala ya wewe kusubiri kupewa pole.

Na nini kingekutokea kama ungemzabua kibao mtoto huyo?


Jibu;


Ghafla ungemwona mtu mzima mwenzako, yawezekana akawa baba wa mtoto au mama wa mtoto. Na kama ni mama atakujia huku akiwa amejifunga kibwaya. Atakuuliza, imekuwaje umpige mtoto wake, na pengine utalipata na tusi la nguoni.


Na kama wewe ni mwanamme, basi, utataka kuonyesha uwanaume wako. Eti utamzabua kibao na mama mtu. Hapo sasa watakuja watu wazima wenzako. Wanaume kama wewe. Utaishia kugalagazwa kwenye matope. Kisa? Umempiga mtoto wa watu na kumdhalilisha mke wa mtu!


Naam, yameshakuwa makubwa hayo. Utatoka hapo ukiwa umechafuliwa haswa. Kile ambacho hukukijua, ni kuwa, mtoto yule aliyekumwagia bakuli la maji machafu katumwa na mtu au watu wazima kama wewe.


Ndio, mwogope mwanadamu. Anapokutafuta atakuwekea mitego mingi. Kama wewe ni mgumu kunasa, basi, atajaribu hata mtego wa kukutumia mtoto akumwagie maji machafu.


Na mwanadamu umeumbwa ili uchafuke. Lililo baya kwa mwanadamu ni kujichafua mwenyewe, lakini, siku zote kuchafuliwa kupo. Nako kuna viwango vyake. Yumkini kila siku inayokwenda kuna mwanadamu mwenzako mahali fulani atasema neno baya la kukuchafua. Ni wanadamu wenzako wasiokutakia mema.


Unapojisikia kuna aliyekuchafua, basi, jitahidi tu upasafishe mwenyewe palipochafuka. Na kama u raia mwema na mwenye adili, basi, jamii nayo imejaa raia wema. Watakusaidia kukusafisha.


Ni Neno Fupi La Usiku Huu. Pasaka Njema.


Maggid Mjengwa,


Iringa.

Jengo la ghorofa 16 laanguka kariakoo

308207 10151505185183058 749260888 n 84a87
ajali-ghorofa 00766
Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde kuwa kuna ghorofa limeanguka eneo la kariakoo jijini Dar es salaam , Habari zaidi zitakujia

source: mjengwa

Friday, March 22, 2013

CHINUA ACHEBE AMEFARIKI DUNIA R.I.P Chinua Achebe.

Photo: R.I.P Chinua Achebe.

Mwandishi mkongwe wa vitabu toka nchini Nigeria. Prof. Chinua Achebe amefariki dunia akiwa nyumbani kwake huko nchini Marekani alipokuwa akiishi akifundisha Brown University .

Prof. Chinua Achebe ambaye amefariki akiwa na miaka 82 inasemekana hivi karibuni amekuwa akihudhuria hospitali mara kwa mara kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua ila hajawekwa wazi.

Vitabu alivyowahi kuandika ni Things Fall Apart, A Man of the People,  Arrow of God,  No Longer at Ease na Anthills of the Savannah.

SOURCE: http://goo.gl/3Ny3J
Mwandishi mkongwe wa vitabu toka nchini Nigeria. Prof. Chinua Achebe amefariki dunia akiwa nyumbani kwake huko nchini Marekani alipokuwa akiishi akifundisha Brown University .

Prof. Chinua Achebe ambaye amefariki akiwa na miaka 82 inasemekana hivi karibuni amekuwa akihudhuria hospitali mara kwa mara kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua ila hajawekwa wazi.

Vitabu alivyowahi kuandika ni Things Fall Apart, A Man of the People, Arrow of God, No Longer at Ease na Anthills of the Savannah.

SOURCE: http://goo.gl/3Ny3J

Papa Francis akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda.