
STAA wa Bongo Movie, Jacob Stephen
maarufu kama JB ameongoza wasanii wengine tisa kujiunga na Chama cha
Mapinduzi (CCM) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya chama hicho
zilizofanyika jijini Mbeya juzi Jumapili. (HM)
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama
hicho, Nape Nnauye aliwatambulisha wasanii hao ambao baadhi yao walikuwa
wamevaa sare za kijani zinazotumiwa na chama hicho, huku akieleza kuwa
wamejiunga CCM baada ya kutambua ubora wa chama hicho.
Kwenye orodha hiyo, wasanii wa filamu walioungana na JB kuwa wanachama wa CCM ni pamoja na Irene Uwoya, Single
Mtambalike 'Richie', Blandina Chagula
'Johari', Tamrina Poshi 'Amanda', Haji Adam 'Baba Haji', Slim Omari,
Salum Haji 'Mboto' na Wastara wakati msanii wa muziki ni Banana Zorro.
"Kabla ya kuanza kwa sherehe yetu
napenda kuwatambulisha wasanii wa filamu na muziki ambao wameamua
kujiunga na CCM leo (jana Jumapili), watakabidhiwa kadi zao baadaye na
Mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete," alisema Nape.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake JB alisema: "Naomba mashabiki wetu wote ambao hawana mapenzi na
CCM watusamehe sana kwa uamuzi wetu wa kujiunga na chama hiki. Tumeona ndiyo sehemu nzuri na tumeamua kujiunga rasmi."
CCM watusamehe sana kwa uamuzi wetu wa kujiunga na chama hiki. Tumeona ndiyo sehemu nzuri na tumeamua kujiunga rasmi."
Naye Wastara alisema: "Tumezaliwa ndani ya CCM, tumekulia CCM na tunaendelea kuishi ndani ya CCM."
Baadhi ya wasanii wengine waliojitosa
kwenye siasa ni pamoja na Joseph Haule maarufu kama Profesa J, Seleman
Msindi 'Afande Sele' na Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, ambaye Mbunge
wa Mbeya Mjini kupitia Chadema.
Chanzo: mwanaspoti
No comments:
Post a Comment