
KIPA wa Simba, Ivo Mapunda amesisitiza
ataendeleza ukali wake kwa wachezaji wote wa Simba anapokuwa uwanjani
ili wazidi kuwa makini kiuchezaji. (HM)
Mapunda alisema: "Mimi huwa nina
mikakati ninapokuwa uwanjani, nataka kuona wachezaji wenzangu wakiwa
makini na kuendana na jinsi mpira unavyochezwa.
"Saa nyingine wanajisahau na ni haki
yangu kuwakumbusha ingawa wanatafsiri kuwa mimi ni mkali lakini ina
faida kwani mwishowe timu inapofungwa anayekuwa wa mwisho golini ni
mimi," alisema.
"Huwa nakua mkali kwa mabeki wangu
nikitaka wawe makini zaidi kwenye mpira, pia wakati mwingine mazingira
yakiwa magumu huwa nawakumbusha viungo na washambuliaji kuwa makini
kwani wanaiweka timu hatarini kwa kiasi fulani wasipokuwa makini.
"Unajua mimi sipendi kufungwa mbali na
timu yangu kupoteza mchezo, naamini kama kina Donald (Mosoti), Owino
(Joseph), Kaze (Gilbert) na mabeki wengine wanakuwa makini basi kila
mchezaji ataonekana bora na timu pia itaonekana bora."
Mara kwa mara Mapunda amekuwa
akiwakaripia wachezaji wenzake hususan wale wa nafasi za beki na kiungo
huku wakati mwingine akiwasukuma akiwataka wakakabe hususan katika
mipira ya kona na adhabu.
Chanzo: mwanaspoti
No comments:
Post a Comment