Sunday, October 28, 2012

JE NI KWELI KUWA MHESHIMIWA DR. JOHN POMBE MAGUFULI NI MSIMAMIAJI WA SERA ZA MAENDELEO NA SIO SIASA?



  • Mheshimiwa Magufuli amekuwa akilalamikiwa sana kwa bomoa bomoa kwa wale wote ambao wamejenga ndani ya hifadhi ya barabara; zoezi hili amekuwa akilifanya kulingana na sheria ya barabara hata wakati fulani bosi wake Mheshimiwa Jakaya Kikwete alimpunguza kasi; je kwa kitendo kama hicho cha kupunguzwa kasi  knatufundisha nini sisi kama wananchi?



  • Daima mheshimiwa Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa yeye hataki kuendekeza siasa katika kuwaletea maendeleo wananchi, je katika siasa za bongo na ushindani wa siasa na uombaji wa kura inawezekana?



  • lakini Namwona Magufuli ni baadhi ya watendaji wachache ambao wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kwa hamu ya kuwaletea maendeleo watanzania, japo pengine hatua hii inaumiza kwani anafanya sivyo vile sisi tunavyofanya bali sheria inavyotaka.


wewe unasemaje Njoo tujadili

1 comment:

  1. Hongera sana Dr.Magufuli utendaji wako pamoja na mapungufu ya kibinadamu utendaji wako ni tanuru kwa taifa tunahitaji viongozi wa namna yako; Hivyo endelea kutuchapia kazi za maendeleo tunakutegemea makubwa zaidi toka kwako;

    ReplyDelete