
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Mwandiga Kigoma.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewataka
wanachama na wakazi wa Kijiji cha Mwandiga kuwa wavumilivu ili aweze
kupambana hadi haki ipatikane.
Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliyofanyika
katika stendi ya mabasi katika Kijiji cha Mwandiga Mkoani Kigoma.
“Wananchi msisikitike kwamba mtoto wenu anaonewa kwa sababu mtoto wenu ni mpambanaji.
Mimi nimevumilia sana mishale ninayorushiwa mimi kama mwanasiasa
mdogo kabisa ni mingi mno, kinachoniuma mimi wananchi wangu ni kwamba
mishale hii narushiwa na wenzangu wa ndani ya chama, hicho ndicho
kinachoniuma, lakini kinachonitia moyo ni nyinyi wanananchi wangu,”
alisema.
Alisema kila akifikiria kukata tamaa anawaza watu wa Kigoma...,
"nasema watu wa Kigoma watasikitika sana acha nipambane na nitapambana,
muhimu ni sharti kutendeka na nitahakikisha haki inatendeka."
Aidha alisema wao walishiriki kujenga chama na wameumia kwa ajili ya chama na watakuwa wa mwisho kutoka.
Alisema alishatoa taarifa ya kwenda kwenye vikao zaidi ya chama,
baraza kuu siri nikujenga demokrasia ambayo inatenda haki, kwa sababu
haiwezekana kila siku kwenye chama kundi moja wao hawakosei na kundi
lingine ndiyo wanakosea kila siku hiyo haiwezekani.
Zitto alisema ni lazima waende kwa utaratibu ule ule kwa sababu wao
wameweka misingi ya hicho chama tukikimbia tutakuwa tunawachia watu
ambao wamekuja badaye, kuja kula matunda ya kazi ambayo wameifanya.
Alisema kuvuliwa nyadhifa zake za chama siyo uahini wala usaliti ni
kwa sababu ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama hicho Taifa na kutaka
matumizi bora ya chama.
Alisema wanachama wa vyama vya siasa wanapojenga uoga kwa viongozi
wao ni udikiteta, lakini viongozi wanapojenga uoga kwa wanachama hiyo
ndiyo demokrasia.
alisema kuna baadhi ya watu wamedhamiria ili avuliwe uanachama wa
chama ili apoteze ubunge “mimi nitarudi kwenu kwa sababu nyinyi ndiyo
mtakaoamua tuendeje na siyo mimi.
Chochote kitakachofanyika na hatua yoyote itakayochukuliwa mimi nitarudi kwenu wananchi wangu”.
SOURCE:
NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment