Monday, December 23, 2013

Yanga: Simba ilistahili ushindi

 
Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro.

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro, amesema wachezaji wa timu yake hawakuwajibika na hawakufuata maelekezo ndiyo maana wakachezea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba juzi walipokutana katika mechi ya kirafiki ya 'Nani Mtani Jembe' iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Minziro, alisema Kikosi cha Yanga kilizidiwa na watani zao Simba kutokana na kila mchezaji kutumia kipaji chake na si kucheza kitimu.

Minziro alisema hali hiyo ndiyo iliwaangusha na kuwapa nafasi wapinzani wao kutawala mchezo.

Alisema wameshayaona mapungufu hayo na sasa watajipanga ili kurekebisha makosa kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

"Wachezaji hawakuwajibika ipasavyo na hawakufuata maelekezo tuliyokuwa tunawapa kila mara, imetuuma sana, tuna timu bora na hatukupaswa kupoteza mechi," alisema Minziro.
Hata hivyo, kipa aliyesimama langoni juzi, Juma Kaseja, hakuwa tayari kuzungumza lolote kuhusiana na matokeo hayo.
Kaseja aliyerejea Yanga kwa mara ya pili, juzi ilikuwa ni mechi yake ya kwanza kuichezea timu yake hiyo mpya baada ya kusajiliwa katika dirisha dogo msimu huu huku akiwa amekaa bila timu tangu Julai Mosi mwaka huu.

Baada ya matokeo hayo, uongozi wa Yanga jana, ulisema utajipanga upya kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na kwamba wanajiandaa na safari ya kwenda nje ya nchi kuweka kambi ili kuweza kuutetea ubingwa wao na kujiandaa na mashindano ya kimataifa.

Klabu hiyo imesema pia bado inaheshimu na inathamini uwezo wa Kaseja licha ya kufungwa mabao matatu jana.

Katika hatu nyingine, Kamati ya Utendaji ya Yanga imesema haikumsajili kipa Juma Kaseja kwa ajili ya kuwafunga 'Wanamsimbazi' huku ikiwapongeza wapinzani zao kwa kucheza soka la kuvutia lililostahili kupata ushindi.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Frank Sanga ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, alisema jijini Dar es Salaam jana, hawakumsajili kipa huyo kuwafunga na kuwakomoa Simba, bali wamemsajili awasaidie kwenye michuano ya kimataifa.

Kamati ya Utendaji ya Yanga ilikuwa inamjibu Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali aliyeushutumu uongozi kwa madai kwamba kumsajili  Kaseja ni makosa makubwa.

Akilimali alikakaririwa usiku wa kuamkia jana akiporomosha maneno makali dhidi ya kipa huyo na uongozi akisema: "mabao mawili kipa wetu (Kaseja) ametoa zawadi. Si mabao ya kufungwa kipa mwenye weledi kama yeye. Nafikiri uongozi ulipaswa kumsajili Ivo Mapunda badala ya Kaseja."

“Huyu mzee (Akilimali) nadhani umri umemzidi, lakini nataka nimkumbushe, huyo Ivo Mapunda aliondoka Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongozi wa wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi zetu (Yanga) dhidi ya Simba," alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaii ya Yanga ambaye alikuwa amefuatana na Sanga.

“Lakini pia nataka nimuulize, wakati Simba inarudisha mabao yote matatu Kaseja alikuwapo langoni? Nadhani hivi vitu si vizuri, tuache kulaumiana tushikamane kwa mustakabali mzuri wa timu,” alisema mjumbe huyo.

Sanga, alisema wanaheshimu uwezo wa Kaseja kwa sababu ndiye kipa aliyedaka mechi nyingi za mashindano ya Afrika kati ya makipa wote nchini, hivyo thamani yake haitashuka kwa kufungwa mabao matatu juzi.

Aidha, Kamati ya Utendaji ilisema mechi ya juzi haikuwa na uzito wowote kwao na ilikuwa sawa na bonanza au fete (michezo ya kubahatisha), hivyo hata kufungwa hakujawaumiza.

“Tuliamua kucheza kumfurahisha  mdhamini, TBL. Tumefungwa lakini bado tunaongoza ligi, hatujapoteza pointi hata moja, ile ilikuwa fete tu,” alisema Sanga ambaye pia alikuwa amefuatana na Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, Beno Njovu.

Kiongozi huyo aliendelea kueleza kuwa Simba walicheza vizuri zaidi ya Yanga juzi na walistahili ushindi, hivyo anawapongeza kwa hilo, pamoja na wadhamini, TBL kwa kuandaa mechi hiyo ya aina yake.

Sanga alisema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Vodacom Tanzania Bara na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika wataimarisha benchi la ufundi na kuboresha timu, huku kukiwa na taarifa zinazodai kwamba kocha Ernie Brandts yuko hatarini kutimuliwa.

Alisema timu itaenda tena kambini Ulaya ili kufufua makali yao kama walivyofanya mapema mwaka huu walipoweka kambi kwenye Hoteli ya Fame Residence iliyopo katika mji wa matanuzi wa Antalya nchini Uturuki.
 
CHANZO: NIPASHE

Sunday, December 22, 2013

Zitto awasihi wananchi kuwa wavumilivu hadi kieleweke

 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Mwandiga Kigoma.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewataka wanachama na wakazi wa Kijiji cha Mwandiga kuwa wavumilivu ili aweze kupambana hadi haki ipatikane.
 
Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika stendi ya mabasi katika Kijiji cha Mwandiga Mkoani Kigoma.
 
“Wananchi msisikitike kwamba mtoto wenu anaonewa kwa sababu mtoto wenu ni mpambanaji. 
 
Mimi nimevumilia sana mishale ninayorushiwa mimi kama mwanasiasa mdogo kabisa ni mingi mno, kinachoniuma mimi wananchi wangu ni kwamba mishale hii narushiwa na wenzangu wa ndani ya chama, hicho ndicho kinachoniuma, lakini kinachonitia moyo ni nyinyi wanananchi wangu,” alisema.
 
Alisema kila akifikiria kukata tamaa anawaza watu wa Kigoma..., "nasema watu wa Kigoma watasikitika sana acha nipambane na nitapambana, muhimu ni sharti kutendeka na nitahakikisha haki inatendeka."
 
Aidha alisema wao walishiriki kujenga chama na wameumia kwa ajili ya chama na watakuwa wa mwisho kutoka. 
 
Alisema alishatoa taarifa ya kwenda kwenye vikao zaidi ya chama, baraza kuu siri nikujenga demokrasia ambayo inatenda haki, kwa sababu haiwezekana kila siku kwenye chama kundi moja wao hawakosei na kundi lingine ndiyo wanakosea kila siku hiyo haiwezekani.
 
Zitto alisema ni lazima waende kwa utaratibu ule ule kwa sababu wao wameweka misingi ya hicho chama tukikimbia tutakuwa tunawachia watu ambao wamekuja badaye, kuja kula matunda ya kazi ambayo wameifanya.
 
Alisema kuvuliwa nyadhifa zake za chama siyo uahini wala usaliti ni kwa sababu ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama hicho Taifa na kutaka matumizi bora ya chama.
 
Alisema wanachama wa vyama vya siasa wanapojenga uoga kwa viongozi wao ni udikiteta, lakini viongozi wanapojenga uoga kwa wanachama hiyo ndiyo demokrasia.
 
alisema kuna baadhi ya watu wamedhamiria ili avuliwe uanachama wa chama ili apoteze ubunge “mimi nitarudi kwenu kwa sababu nyinyi ndiyo mtakaoamua tuendeje na siyo mimi. 
 
Chochote kitakachofanyika na hatua yoyote itakayochukuliwa mimi nitarudi kwenu wananchi wangu”.
 
SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

SIMBA NDIYE MTANI JEMBE,YAIONESHA SOKA YANGA, YAICHAPA 3-1

 Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana.
 Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Yanga.
 Benchi la ufundi la timu ya Simba.
Benchi la Ufundi la Yanga.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu yao.
 Raha ya ushindi.
 Furaha kwa Simba.

 Hamisi Kiiza akitafuta mbinu za kumtoka, Ramadhani singano.
 Ivo Mapunda akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea uwanjani baada ya kuchapwa 3-1 na watani zao wa jadi Simba.
 Juma Kaseja akibembelezwa na Mbuyu Twite baada ya kusababisha 
 Mmoja wa mashabiki wa Yanga akitolewa nje baada ya kuzimia uwanjani.
 Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Simba.
 Wachezaji wa akiba wa Simba  wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho. 
 Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 3-1.
 Wachezaji wa Simba wakimnyanyua juu kocha wao, Zdravko Logarusic mara baada ya kumalizika kwa mchezo maalumu wa Nani Mtani Jembe uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-1.




 Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe akimkabidhi kombe nahodha wa Simba Haruna Shamte.


Wednesday, December 11, 2013

Hotuba ya Barack Obama, rais wa Marekani kwenye mazishi ya kitaifa ya Nelson Mandela

18_obama_lg_4c7a8.jpg

Na Fadhy Mtanga

Jumanne, Disemba 10, 2013
Kwa Graça Machel na familia ya Mandela; kwa Rais Zuma na wajumbe wengine wa serikali; kwa wakuu wa nchi na serikali, waliopita na waliopo sasa, wageni wengine waalikwa – ni heshima ya kipekee mno kuwa nanyi leo, kusherehekea maisha yasiyo na kifani. Kwa watu wa Afrika Kusini – watu wa kila rangi na kila mfumo wa maisha – dunia inawashukuruni sana kwa kutushirikisha Nelson Mandela. Mapambano yake yalikuwa mapambano yenu. Shangwe yake ikawa shangwe yenu. Utu wenu na matumaini vilielezwa kupitia maisha yake, na uhuru wenu, na demokrasia yenu ni urithi wake uliotunzwa vema.

Ni vigumu kumsifu sana mtu yeyote – kuweza kudaka maneno na siyo matendo na nyakati zilizoyafanya maisha yake, lakini kupata ukweli muhimu umhusuo – furaha yake binafsi na huzuni; nyakati tulivu na ubora wa kipekee ulioiangaza nafsi ya mtu. Ni ngumu mno kwa gwiji katika historia, aliyelipeleka taifa katika haki, na katika mchakato uliowahuisha mabilioni ya watu ulimwenguni.

Aliyezaliwa wakati wa vita ya kwanza ya dunia, mbali kabisa kutoka mataifa yaliyokuwa na nguvu, mvulana mdogo aliyekuwa akichunga ng'ombe na kufundishwa na wazee wake wa kabila lake la Thembu – Madiba aliweza kuibuka kama mkombozi wa mwisho wa karne ya 20. Kama ilivyokuwa Ghandhi, aliongoza mapambano – harakati ambazo mwanzo wake ulionesha nuru ndogo ya mafanikio. Kama King, alipaza sauti yake ya manung'uniko ya wanaokandamizwa, na uadilifu muhimu wa haki kwa kila rangi. Alipambana na kifungo cha kikatili kilichoanza wakati wa Kennedy na Khrushchev, kilichokwenda hadi nyakati za mwisho za Vita Baridi. Aliibuka kutoka jela, pasipo kutumia nguvu ya bunduki, akaweza – kama Lincoln – kuileta nchi yake pamoja ilipokuwa katika hatari ya kuvunjika vipandevipande. Kama waasisi wa Amerika, aliweka misingi ya kikatiba ya kuhifadhi uhuru kwa ajili ya vizazi vijavyo – kujitolea kwa ajili ya demokrasia na utawala wa sheria ulioridhiwa si tu na uchaguzi uliomweka madarakani bali na hiyari yake ya kuachia madaraka.(P.T)

Kwa kuondoka kwake, na kwa mapenzi aliyoyapata akiyastahili, inashawishi kumkumbuka kama alama, yenye tabasamu na iliyotakata, iliyojiepusha na maovu ya wengine wasio na utu. Lakini Madiba mwenyewe alikataa kwa nguvu zote taswira isiyo na maana. Badala yake, alisisitiza katika kushiriki nasi mashaka yake na hofu yake; makosa yake sambamba na kushinda kwake. "Mimi si mtakatifu," alisema, "isipokuwa kama mnanidhania mtakatifu mwenye dhambi asiyeacha kujaribu."

Ni kwa sababu tu alikubali kuwa na mapungufu – kwa kuwa alijaa ucheshi, hata kukosea, licha ya mizigo mizito aliyokuwa ameibeba – nasi tukampenda vivyo hivyo. Hakuwa mtu aliyetengenezwa kwa marumaru; alikuwa binadamu wa kawaida – mtoto na mume, baba na rafiki. Hayo yote yanaonesha ni kwa nini tumejifunza mengi sana kutoka kwake; na ndiyo sababu bado tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake. Kila alichokipata hakikuepukika. Katika utao wa maisha yake, tunamwona mtu aliyeiweka nafasi yake kwenye historia kwa kupitia mapambano na werevu; msimamo na imani. Ametuambia nini kinachowezekana si tu kwa kupitia kurasa zenye vumbi za vitabu vya historia, bali pia kwa kupitia maisha yetu wenyewe.

Mandela ametuonesha nguvu ya matendo, kukabiliana na hatari kwa ajili ya ukamilifu wetu. Pengine, Madiba alikuwa sahihi kusema amerithi, "ukaidi wa kujivunia, utukutu katika haki" kutoka kwa baba yake. Kwa yakini ameshiriki na mamilioni ya Waafrika Kusini weusi na wengine wa rangi mchanganyiko hasira ya kuzaliwa katika "maelfu ya twezo, maelfu ya vitendo vilivyokosa utu, maelfu ya nyakati zisizokumbukika.....matamanio ya kupambana na mfumo uliowafunga watu wangu".

Lakini kama manguli wengine wa ANC – akina Sisulu na akina Tambo – Madiba alikuwa na nidhamu ya hasira yake; akayapeleka matamanio yake ya mapambano kitaasisi, na katika ulingo, na kwa mikakati mahsusi, kwamba waume na wake wangeweza kusimama kwa ajili ya utu wao. Vilevile, akayakubali madhara ya matendo yake, akifahamu kuwa kusimamia haki na usawa kuna gharama zake. "Nimepambana dhidi ya ukandamizaji wa watu weupe na nimepambana dhidi ya ukandamizaji wa watu weusi," aliyasema hayo katika kesi yake ya mwaka 1964. "Nimeutukuza ukamilifu wa demokrasia na jamii huru ambapo watu wote huishi kwa pamoja katika maelewano na fursa sawa. Ni imani ninayoishi nayo nikitumaini kuipata. Lakini ikihitajika, ni imani niliyojiandaa kuifia."

Mandela ametufundisha nguvu ya matendo, lakini pia mawazo; umuhimu wa kuwa na sababu na hoja; umuhimu wa kuwasoma siyo tu wale unaokubaliana nao, bali pia wale usiokubaliana nao. Alifahamu mawazo hayawezi kuhifadhiwa ndani ya kuta za jela, ama kuondoshwa kwa risasi ya mdunguaji. Akaigeuza kesi yake kuwa mashitaka rasmi dhidi ya ubaguzi wa rangi kwa kupitia uzungumzaji wake na hisia kali, pia kwa kupitia mafunzo yake kama wakili. Akaitumia miongo ndani ya jela kunoa uwezo wake wa kujenga hoja, lakini pia kueneza kiu yake ya maarifa kwa wengine katika harakati za mapambano. Akajifunza lugha na tamaduni za wakandamizaji wake ili siku moja aweze kuwaonesha ni kwa kiasi gani uhuru wao ulitegemea pia uhuru wake.

Mandela alionesha kuwa matendo na mawazo pekee havitoshelezi; haijalishi ni sahihi kwa kiasi gani, vinatakiwa kuwa kisheria na kitaasisi. Alikuwa mtu wa vitendo, akazijaribu imani zake dhidi ya mazingira magumu na historia iliyokuwepo. Katika kanuni ya msingi hakukubali kushindwa, hicho kilipelekea akatae kuachiwa huru kwa masharti, akiukumbusha utawala wa kibaguzi kuwa, "kamwe mfungwa haingii katika mikataba". Lakini alionesha katika majadiliano magumu nia ya kupeana madaraka na kuandika sheria mpya, hakuogopa kufikia maridhiano kwa malengo makubwa. Na kwa kuwa hakuwa pekee yake kama kiongozi wa harakati, lakini akiwa mwanasiasa mweledi, katiba iliyoandikwa ikawa yenye kuthamini demorasia ya rangi tofauti; ikiweka bayana maono yake juu ya sheria inayolinda haki za wachache na za wengi pia, na uhuru wa tunu kwa kila Mwafrika Kusini.
Hatimaye, Mandela alielewa juu ya mambo yanayoiunganisha roho ya mwanadamu. Kuna neno Afrika Kusini – Ubuntu – linaloelezea hiba yake kubwa: kutambua kwake kuwa sisi sote tunaunganishwa katika namna mbalimbali ambazo zinaweza kutoonekana kwa macho; ambazo zinaonesha u-moja kwa binadamu; kwamba tunakuwa sisi kwa kushirikisha wengine katika u-sisi, na kuwajali wale wengine wanaotuzunguka. Hatuwezi kufahamu ni kwa kiwango gani hii ilikuwa ndani yake, ama kwa kiasi gani ilichochewa na kung'arishwa katika selo yenye kiza na upweke. Lakini tunakumbuka ishara ya mwili wake, kwa ukubwa na udogo wake – akiwatambulisha mabwana jela wake kama wageni wa heshima siku aliyoapishwa; ndani ya sare ya Springbok; akiigeukia familia yake akiihamasisha kupambana na VVU/UKIMWI – ikionesha kiwango cha juu cha huruma yake na uelewa. Si tu alikolezwa na Ubuntu; bali aliwafundisha wengi kuitafuta kweli ndani yao. Ilimchukua mtu kama Madiba kumkomboa si tu mfungwa, bali na bwana jela pia; kuonesha kuwa unapaswa kuwaamini wengine ili nao waweze kukuamini wewe; kufundisha kuwa maridhiano hayamaanishi kuyadharau machungu yaliyopita, bali kumaanisha kupambana nayo kwa ushirikishaji, ukarimu na ukweli. Alizibadili sheria, lakini na mioyo pia.

Kwa watu wa Afrika Kusini, kwa wale wote aliowapa msukumo kote ulimwenguni – kufariki kwa Madiba ni wakati hasa wa maombolezo, na pia wakati wa kuyasherehekea maisha yake ya kishujaa. Lakini ninaamini inapaswa pia kutupa wasaa wa kujitathimini wenyewe. Kwa uaminifu, pasipo kujali mahali tulipo ama hali tulizo nazo, shurti tujiulize: kwa namna gani ninayatekeleza mafunzo yake kwenye maisha yangu mwenyewe?

Ni swali ninalojiuliza mwenyewe – kama binadamu na kama rais. Tunafahamu kama ilivyo Afrika Kusini, Amerika ililazimika kupambana na karne za ubaguzi wa rangi. Kama ukweli ulivyo hapa, iliwachukua watu wasiohesabika kujitoa mhanga – wanaojulikana na wasiojulikana – kuleta mapambazuko ya siku mpya. Michelle pamoja nami ni wanufaishwa wa mapambano hayo. Lakini ndani ya Amerika na Afrika Kusini, na nchi zingine kote ulimwenguni, hatuwezi kuruhusu maendeleo yetu kuufunika ukweli kuwa kazi yetu haijafanywa. Mapambano yanayofuatia ushindi juu ya usawa na haki za kiraia kote ulimwenguni yanaweza yasitoshelezwe uadilifu na unyoofu ukilinganisha na yale yaliyotangulia, lakini haimaanishi umuhimu kidogo. Kwa dunia ya leo, tungali tukiwaona watoto wakiteswa na njaa, na magonjwa; kukosa shule, na matarajio yao machache kwa maisha ya baadaye. Duniani kote leo, wake na waume wangali wakifungwa kwa ajili ya imani zao kisiasa; na wangali wakiadhibiwa kwa vile waonekanavyo, ama vile waabuduvyo, ama nani wawapendao.

Sisi, pia, lazima tutende kwa ajili ya haki. Sisi, pia, lazima tutende kwa ajili ya amani. Wapo wengi mno miongoni mwetu ambao kwa furaha tunaukumbatia urithi wa Madiba katika maridhiano ya rangi, lakini kwa hisia kali tunayakataa mabadiliko ya wastani ambayo yangeshindana na umasikini sugu na kukosekana kwa usawa kunakokua. Wapo viongozi wengi mno wanaodai kushikamana na mapambano ya uhuru ya Madiba, ilhali hawavumilii maoni tofauti kutoka kwa watu wao wenyewe. Na wapo wengi wetu wanaosimama pembeni, wakistarehe katika kuridhika ama wakizidharau sauti zetu zinapolazimika kusikika.
Maswali tunayokumbana nayo leo – tukuze vipi usawa na haki; tuulinde vipi uhuru na haki za kibinadamu; tukomeshe vipi migogoro na vita vya wenyewe – hayana majibu rahisi. Lakini hakukuwa na majibu rahisi mbele ya mtoto yule pale Qunu. Nelson Mandela anatukumbusha kuwa daima huonekana haiwezekani hadi jambo linapotendwa. Afrika Kusini inatuonesha kuwa hivyo ni kweli. Afrika Kusini inatuonesha tunaweza kubadilika. Tunaweza kuchagua kuishi katika dunia isiyotafsiriwa kwa tofauti zetu, bali kwa matumaini yetu yanayofanana. Tunaweza kuichagua dunia isiyotafsiriwa kwa mgogoro, bali kwa amani na haki na fursa.

Hatutowaona watu kama Nelson Mandela tena. Lakini wacha mimi niseme kwa vijana wadogo wa Afrika, na vijana wadogo kote ulimwenguni – mnaweza kuyafanya maisha yake yakafanya kazi ndani yenu. Zaidi ya miaka thelathini iliyopita, nikiwa bado mwanafunzi, nilijifunza kuhusu Mandela na mapambano katika nchi yake. Ilichochea kitu ndani yangu. Iliniamsha katika wajibu wangu – kwa wengine, na kwa nafsi yangu -

- na kuniweka katika safari isiyoyumkinika ambayo imenifikisha hapa leo. Na wakati sitoufikia mfano wa Madiba, ananifanya nitake kuwa bora. Anazungumza kilicho bora ndani yetu. Baada ya huyu mkombozi mufti kupumzishwa; baada ya sisi kurudi kwenye majiji yetu na vijiji vyetu, na kurejea mizunguko yetu ya kila siku, ni vema tuitafute nguvu yake – kwa ukuu wa roho yake – mahali fulani ndani yetu. Na wakati giza likiingia usiku, wakati ukosefu wa haki ukituelemea mioyoni mwetu, mikakati yetu kutofanikiwa – tumfikirie Madiba, na maneno yaliyomletea faraja ndani ya kuta nne za selo yake:
Haijalishi namna mashaka yalivyoniandama,
Namna nilivyoshtakiwa na adhabu ndefu,
Mimi ndiye mwamuzi wa majaaliwa yangu,
Mimi ndiye nahodha wa nafsi yangu.

Ni nafsi kuu kwa kiasi gani. Tutamkumbuka mno. Mwenyezi Mungu aibariki kumbukumbu ya Nelson Mandela. Mwenyezi Mungu awabariki watu wa Afrika Kusini.

Imetafsiriwa katika Kiswahili na Fadhy Mtanga

source: mjengwa blog

Rais Kikwete na Mama Salma walipokuwa na Mzee Mandela.


DSC04695 22626
DSC04697 d7d46
DSC04700 2704a
DSC04704 8c2c3
source: mjengwa bvlog

Tuesday, November 12, 2013

Uchunguzi Kompyuta ya Mvungi kiza Kinene

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani), mapanga matano yanayodaiwa kutumika kumjeruhi Dk. Sengondo Mvungi, baada ya kuvamiwa nyumbani kwake eneo la Kibamba, nje kidogo ya Jiji la Dares Salaam na wanaosadikiwa kuwa majambazi. Wa pili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi.(PICHA: OMAR FUNGO)
Jeshi la Polisi limetangaza kuongezeka kwa watuhumiwa wa tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi, bila kueleza kompyuta mpakato (laptop) yake aliyoporwa kama imepatikana ama la.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, walizungumza na waandishi wa habari jana kuelezea mwenendo wa upelelezi wa tukio hilo huku wakisema watuhumiwa watatu zaidi wametiwa mbaroni.

Waziri Nchimbi alisema upelelezi umefikia asilimia 80 na watuhumiwa tisa wamekwisha kukamatwa na vielelezo mbalimbali. Kabla ya jana, Jeshi hili lilitangaza kukamata watuhumiwa sita.

Kova aliwataja watuhumiwa na vielelezo walivyokamatwa navyo kuwa ni mapanga matano na simu aina ya Nokia iliyoporwa nyumbani kwa Dk. Mvungi.

Hata hivyo, Dk. Nchimbi na Kova walisema upelelezi wa kina unaendelea juu ya kompyuta ya Dk. Mvungi na kwamba baada ya muda mfupi taarifa kamili itatolewa.

Dk. Mvungi ambaye ni mwanasheria mkongwe aliyebobea katika masuala ya sheria na katiba, alihamishiwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

Kuna hisia kwa baadhi ya watu kwamba huenda alifavamiwa nyumbani kwake kwa hisia kuwa wajumbe wa tume hiyo wanalipwa fedha nyingi na hivyo kulikuwa na uwezekano wa kuwa na fedha nyingi nyumbani kwake.

Hata hivyo, pamoja na hisia hizo, pia kuna hofu miongoni mwa jamii kuwa huenda alijeruhiwa na kuporwa laptop yake ambayo ilikuwa na taarifa muhimu na nyeti kuhusu mchakato mzima wa Katiba Mpya na taarifa hizo zitakuwa mikononi mwa watu wasiostahili.

Hofu hiyo inatokana na ukweli kwamba miongoni mwa vitu vilivyoporwa nyumbani kwa Dk. Mvungi, Mbezi Msakuzi baada ya kupigwa mapanga na majambazi hao ni laptop ambayo ni moja ya nyenzo zake muhimu za kazi.

Hofu hii inaelezwa kutanda ndani ya Tume kwa kuwa mbali ya kuwako na uwezekano huo, kwa kuwa Dk. Mvungi amebobea katika masuala ya katiba alikuwa nguzo muhimu kwa Tume hasa katika kipindi hiki cha mwisho cha kuandaa rasimu ya mwisho ya Katiba Mpya.

Katika mkutano wa jana, Dk. Nchimbi alisema Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha intelijensia lilifanikiwa kuwakamata wahalifu hao ambao walionyesha vifaa walivyotumia ambavyo ni mapanga matano na kigoda kimoja.

Dk. Nchimbi alisema kwa asilimia 80 upelelezi wa tukio hilo umekamilika kwa watumuhumiwa na vilelezo muhimu vimepatikana na wakati wowote watafikishwa mahakamani.

Kamanda Kova alidai kuwa watuhumiwa hao ni Msigwa Mpopela (30) kwa jina maarufu Matonya mkazi wa Vingunguti na ambaye kabla ya tukio alikuwa fundi ujenzi nyumbani kwa Dk. Mvungi.

Alidai Mpopela na mtuhumiwa mwingine Chabago Magozi ndiyo vinara wa uhalifu huo na kwamba baada ya kukamatwa walitaja wenzao na silaha walizotumia na kukamatwa na simu aina ya Nokia ambayo iliporwa nyumbani kwa Dk. Mvungi.

Wengine ni Ahemed Ally (40) maarufu kama Khatibu mkazi wa Mwananyamala; Zakaria Rafael Masesa (25), mkazi wa Buguruni Mlapa ambaye ni dereva bodaboda na Longushi Semaliko Losingo (29), mfanyabashara wa ugoro mkazi wa Msimbazi.

Wengine ni Paul Yamusi (29), Juma Hamisi (29) maarufu Kangua Mnanda Saluwa (40) kwa jina maarufu White au Mlewa wote wakazi wa Vingunguti.

Kova alisema jalada la kesi iliyo limefikishwa kwa mwanasheria wa serikali ili kuona kama kuna kesi dhidi yao na kuwa ikibainika watafikishwa mahakamani.

Aidha, alisema watuhumiwa hao walikamatwa kwa haraka kutokana na ushirikiano kutoka familia ya Dk. Mvungi na vyombo vya habari kutoandika sana.

Dk. Mvungi, aliyewahi kuwa Mhadhiri Mwandamizi Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alipatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia Novemba 4, mwaka huu nyumbani kwake Mbezi Msakuzi, Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE

Saturday, October 5, 2013

PRESIDENT OBAMA AND VICE PRESIDENT BIDEN TAKING A WALK


Rais Obama aenda zake mtaani kununua sandwich


Picture
Rais wa Marekani, Barack Obama akikatiza katika maungio ya barabara ya 17 na Pennsylvania Avenue jijini Washington, D.C., baada ya kutoka kwenye mgahawa wa mtaa wa jirani kununua 'sandwich' tarehe 4 Oktoba 2013. (picha: Pete Souza/ Ikulu "White House"). Wawakilishi wa Wananchi huko Bungeni 'wamemwekea usiku' na 'kumzingua' Rais Obama kwenye mipango yake inayotegemea bajeti ambayo waligoma kuipitisha, naye akatilia ngumu kubadili au kuondoa miradi yake.
 

source: wavuti.com