(PICHA: Dastun Shekidele/GPL Morogoro)
source: global publishers
Jana (Ijumaa) jioni Kuambiana na wasanii wenzake walikuwa baa wakinywa pombe hadi usiku mnene lakini bado aliendelea kulalamikia maumivu ya tumbo.Wenzake walimuuliza ni kwa nini alikuwa akiendelea kunywa pombe kama anaumwa? Akawaambia wamuache!Baada ya kumaliza kunywa kila mmoja alikwenda kulala chumbani kwake huku tukiahidiana kwamba itakapofika saa 3:00 asubuhi tuwe tayari kwa ajili ya kwenda ‘location’.Lakini ulipofika muda huo sisi tukiwa tayari kwa safari tulikwenda kugonga mlango wa chumba chake bila mafanikio.Cha kushangaza, alisikika sauti yake kwa mbali. Kwa bahati nzuri mlango ulikuwa wazi, mmoja akaingia ndani na kumkuta ameanguka chooni na hajiwezi. Neno lake la mwisho alisema kwamba anajisikia kuishiwa nguvu na anaharisha damu.Kutokana na hali yake hiyo mbaya tulimbeba na kumlaza kitandani kisha tukatafuta gari na kumkimbiza Hospitali ya Mama Ngoma ambapo daktari alisema kwamba alishafariki dunia muda mrefu.
Kwa kawaida, mtu kuharisha damu kwa sababu ya vidonda vya tumbo inawezekana kabisa, hiyo kitaalam inaitwa heamatemesis. Inatokana na perforation ya tumbo yaani kidonda kuwa kikubwa.
Kwa mtumiaji wa pombe ni kipindi anatakiwa kusimama au kuacha moja kwa moja. Kama hatajali afya yake anaweza kufa ghafla kwani uwezekano wa utumbo kukatika ghafla ni mkubwa.
Nimeumia sana kwani hii filamu ndiyo ilikuwa apate fedha nyingi sana kwa sababu ni ya kwake mwenyewe na ni kali mno, amecheza vizuri akinishirikisha mimi.Lakini ndiyo hivyo tena imeishia katikati, sijui ni nani atakayeiendeleza maana mwenyewe katuachia majonzi yasiyoelezeka