
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Zanzibar na
kuwaambia CCM itasimamia haki za Wazanzibar na kuhakikisha Muungano
unadumu na Mapinduzi ya Zanzibar yanaenziwa .

Wananchi wakionyesha ishara ya Serikali mbili kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar.

Kila mtu alionyesha mapenzi yake kwa CCM.

Wakazi wa Zanzibar hawakujali mvua iliyokuwa inanyesha kwenye mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar

Mama
Fatma Karume akihutubia wakazi wa Unguja na kuwaambia kuwa waasisi wetu
waliweka uzio wa kutulinda na kudumisha umoja na undugu wetu na kusema
uzio huo ni Muungano wetu.

Mbunge wa
Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Unguja kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti na kuwataka wananchi hao
kuwa makini na viongozi wanaogeuza maneno huku akitolea mfano kutoka
kwenye kitabu cha Maalim Seif.

Sehemu ya
Umati uliohudhuria mkutano wa hadhara ambao ulihutubiwa na Viongozi
mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana. (FS)
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment