Friday, December 21, 2012

Thursday, December 20, 2012

HII INATISHA TUTAJINASUA VIPI NA HALI HII


Kondakta wa Daladala akiwa amekaa pembezoni mwa barabara ya Morogoro eneo la Kimara Bucha kutokana na foleni kubwa iliyoanzia Kimara Stopover hadi Ubungo Mtaa jijini Dar es Salaam jana na iliyosababisha kero kwa watumiaji wa barabara hiyo. (Picha na Fidelis Felix/MWANANCHI)


Source: 
http://www.wavuti.com

Sunday, December 16, 2012

MHESHIMIWA UNAKUMBUKA CHUMBA NA KITANDA HIKI?



Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitembelea bweni namba 15 ambamo Rais Kikwete alikuwa akiishi wakati akiwa mafunzoni hapo  katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha,jana Jumamosi Desemba 15, 2012 kabla ya kuwakutunuku kamisheni maafisa hao 192 waliohitimu chuoni hapo.

picha na ikulu

MTOTO JASIRI SAFI SANA




..Mheshimiwa Rais naomba kukupiga picha msichana Shalom anamwambia Amiri Jeshi  Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete   katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Arusha, leo Jumamosi Desemba 15, 2012 baada ya kuwakutunuku kamisheni maafisa hao 192 waliohitimu chuoni hapo.

PICHA NA IKULU

Monday, December 10, 2012

MIAKA 51 YA UHURU TUMETOKA MBALI



Leo ni siku ya Uhuru wa Taifa lililokuwa likijulikana kama Tanganyika na hatimaye baada ya kuungana na Zanzibar mwaka 1964 likawa sehemu ya nchi tunayoifahamu hivi leo kama Tanzania.

Unaowaona hapo juu kwenye picha ni viongozi ambao mpaka sasa wameiongoza Tanzania.Kutoka kushoto kuna muasisi wa taifa,Baba wa Taifa,Hayati Julius Kambarage Nyerere, kisha Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Rais wa sasa, Jakaya Mrisho Kikwete.

HAPPY INDEPENDENCE DAY TANGANYIKANS!

Thursday, December 6, 2012

Tanzania is Still the Second Least Corrupt Country in East Africa After Rwanda



Tanzanians feel government officials are much more corrupt this year than they were last year, according to a global survey published yesterday.Tanzania dropped two places to 102nd in Transparency International’s Corruption Perceptions Index 2012, which has listed 174 countries.

“This means the public sector is perceived by the people as more corrupt this year than it was last year. The bigger the number of the rank the more corrupt the country is,” the report says.However, Tanzania is still the second least corrupt country in East Africa after Rwanda. Burundi is the most corrupt country in the region, followed by Kenya and Uganda.

Rwanda retains its status as the region’s least corrupt country despite dropping one place in the global rankings to 50th.Uganda, Kenya and Burundi have climbed to 130th, 139th and 165th from 143rd, 154th and 172nd, respectively.

Tuesday, December 4, 2012

KUTOKA KWENYE UKURASA WA MH.EDWARD LOWASSA KATIKA FACEBOOK





KAZI NI MSINGI WA MAENDELEO KWA KILA TAIFA LILILO PIGA HATUA, Ewe Kijana mzalendo wa taifa hili chapa kazi ujenge heshima yako na heshima ya Taifa letu…Huu si wakati wa KIJANA kulalamika ni wakati wa KIJANA kuchapa kazi…

source: bongocelebrity.com

Monday, December 3, 2012

NIMEIPENDA HII YA MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mlemavu Bwana Mwendo Saidi katika kijiji cha Mandawa wilaya ya Lindi vijijini jana wakati Rais aliposimama kwa muda kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho ili kujua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili.Mlemavu huyo alimweleza Mheshimiwa Rais Kuwa yeye na wenzake wawili wanaomba wapatiwe Bajaji ili kuanzisha mradi utakaowawezesha kujikimu kimaisha.Mheshimiwa Rais Kikwete aliridhia ombi hilo na kuahidi kutoa msaada huo mara moja.Rais Kikwete yupo mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha na 

Freddy Maro-IKULU