Monday, December 3, 2012

NIMEIPENDA HII YA MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mlemavu Bwana Mwendo Saidi katika kijiji cha Mandawa wilaya ya Lindi vijijini jana wakati Rais aliposimama kwa muda kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho ili kujua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili.Mlemavu huyo alimweleza Mheshimiwa Rais Kuwa yeye na wenzake wawili wanaomba wapatiwe Bajaji ili kuanzisha mradi utakaowawezesha kujikimu kimaisha.Mheshimiwa Rais Kikwete aliridhia ombi hilo na kuahidi kutoa msaada huo mara moja.Rais Kikwete yupo mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha na 

Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment