Wednesday, January 30, 2013

Saturday, January 19, 2013

Wednesday, January 16, 2013

HII IMEKAAJE?


MICHEZO NI AFYA

Usije kujiona umeshapita wakati wa kufanya mazoezi bado muda na wakati unakuruhusu kujiweka  mwili kiafya ukiona picha hii unaweza kugundua kuwa wakati unao na mazoezi hayanana umri

SOURCE VIJIMAMBO

Monday, January 14, 2013

BONGO DAR-ES-SALAAM UTAIPENDA TUU


Mchakato wa utengenezaji barabara za kisasa kupitia morogoro road hadi lango la jiji ukikamilika utakuwa na mwonekano huu.
Morogoro road hiyo itakuwa bomba na pindi itakavyo kamilika hii ndiyo taswira ya muonekano wake
Mabasi yatakayo tumia barabara hizo maalum ndiyo haya

source vijimambo

AFANDE SELE: NANI ATABAKI MIKOANI??? KAMA KILA KITU KIPO DAR ES SALAAM



Na Selemani Msindi 'Afande Sele', Morogoro

Wanalalamika kila siku Chinga kukimbilia Dar-es-Salaam na ongezeko la watu dsm, foleni halafu bado kila kitu wanataka walundike Dsm. Sasa nani atabaki Mikoani? Afanye nini Lindi, Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Iringa, Singida, Mara n.k kama kila kitu kipo Dsm?

Ukistajabu ya Musa .... Kila siku viongozi wa Serikali wanalalamika kwamba wamachinga/vijana mikoani kukimbilia DSM ni tatizo la kitaifa au ni bomu hatari kwa amani ya Taifa, ila kila siku wanajenga na kubomoa miundo mbinu ya Jiji la Dsm ili kukabiliana na foleni, misongamano ya watu na makazi kwa kuwa ongezeko la watu Dsm linakua maradufu kila mwaka na yote ni kwa sababu nyanja kuu za ajira/uchumi kwa kiasi kikubwa zipo Dsm. Watu wengi huja Dsm sasa kitu cha ajabu;

Bado viongozi wa Serikali tena Wasomi wakubwa (Maprofesa/madokta) hawalioni hilo tatizo kama ni tatizo ambalo hata asiejua kusoma/kuandika analiona lakini wao hawaoni wanazidi kulazimisha kila kitu kiwe DSM, nani atabaki Kigoma, Lindi, Mtwara, Singida n.k afanye nini?

Cha ajabu wanawabeza wananchi wa Lindi na Mtwara ni wapuuzi/wahaini wa kupuuzwa wajinga wasiojielewa kwa kukosa shukrani, eti wamepewa umeme wa megawati 18, hawawezi kuutumia kwa lolote, watautumia ikiwa mumeua viwanda vya Korosho Lindi na Mtwara, Mumeua Mashamba ya Mkonge Lindi, Karanga Nachingwea, mnawakopa Korosho na Ufuta hamuwalipi kwa wakati, hawapati pembejeo za kilimo kama inavyostahili, ni dhambi kubwa kuwaita wapuuzi, hawakatai Umeme unaotokana na Gesi ya kusini kutumika Tanzania nzima! 

Ndani ya Miaka 50 ya Uhuru mmeshindwa kuwawekea barabara mpaka leo inasuasua haijaisha ni kama km 500 tu, Mnajua kuzorota kwa uchumi wa mikoa ya Kusini ni kutokana na kutumika kwake kwenye Ukombozi wa Nchi za kusini mwa Afrika! Msumbiji, South Afrika, Angola n.k.. Katika mwaka wa uchumi unaoishia Novemba Korosho imeingizi Dola za Kimarekani Milioni 151, pamba dola za kimarekani Milioni 53... licha ya zao la korosho kuliingizia taifa kiasi cha shilingi trilioni 7.2, ndiyo mikoa iliyo nyuma kimaendeleo katika miaka 51 ya uhuru.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

source habari na matukio blog

JE KUWA MSOMI NI UFUMBUZI WA KUPAPAMBANUA MAMBO?



Wanafunzi wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) 

Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na ikielekea Kigamboni





Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue.Picha Zote na Habari na Mdau

SOURCE HAKI NGOWI BLOG

Thursday, January 10, 2013

MAWAZIRI WAWILI WACHAPA KAZI: TUNGEKUWA NA WENGINE KUMI WA MFANO WAO NCHI INGESONGA MBELE;


Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia) na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe wakiongea wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Tabora leo Januari 10, 2013.
SOURCE IKULU

Tuesday, January 8, 2013

DU BADO TUNASAFARI NDEFU PAMOJA NA UTAJIRI WOTE WA MKOA WA MWANZA


DARAJA LINALOKARIBIA KUCHUKUA ROHO ZA WATU NA SERIKALI IKO TULII


Wakati serikali ikiahidi kukamilisha ujenzi wa madaraja yapatayo 10 sehemu mbalimbali nchini huku ujenzi na ufunguzi wa madaraja hayo ukiendelea kufanyika hali iko hivi katika daraja la Sukuma lililopo katika barabara kuu inayounganisha vijiji vya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.
Daraja hili mbao zake zimesagika kabisa kiasi cha kufanya magari yanayopita kutumia daraja hili muhimu kupita kwa mwendo wa kusuasua yakihofia kukumbwa na maafa. 
Mbao zilizo chomoka zimeegeshwa tu, mawe yametumika kuziba mashimo ya uwazi kati ya nondo na nondo hii ni hatari si kwa magari tu bali hata kwa waendao kwa miguu hali inayosababisha hata waendeshao baskeli kushuka na kuzikokota baiskeli zao wakihofia usalama wao.
SOURCE vijimambo blog

Monday, January 7, 2013

CHADEMA NAUSHAURI WAO KUHUSU KATIBA MPYA TANZANIA


Picture
Picture

Mmoja wa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya chama chake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam


Source: http://www.wavuti.com

MMMMMMM ITAWEZEKANA?



SOURCE HAKI NGOWI BLOG

KUMBE NA MHESHIMIWA DR.JOHN POMBE MAGUFULI NAYE YUMO KUMBE?


ig5 1 97c45
Waziri wa Ujenzi,Dk. John Magufuli akipiga Ngoma aina ya Tumba sambamba na Mpiga Gita wa Bendi ya Msondo Ngoma wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Mbutu,Wilayani Igunga Mkoani Tabora leo.Uzinduzi huo umefanya na Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani).Picha na IKULU

Thursday, January 3, 2013

Sajuki ametutupa mkono


“MUME wangu amefariki dunia.” Haya ni maneno ya Wastara Juma, mke wa Sadick Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki, aliyefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Baada ya maneno hayo aliyoyatuma kwa mwandishi wa habari hii kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, Wastara hakupokea simu yake iliyokuwa ikiita mara kadhaa kutaka ufafanuzi zaidi.
Sajuki ambaye hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharimia matibabu yake,  alifariki dunia jana alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa kwa matibabu.
Alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, akisubiri kusafiri kwenda India kwa mara nyingine, kuendelea na matibabu
Alianguka jukwaani
Kabla ya kulazwaDesemba 18 mwaka jana, Sajuki alifikishwa hospitalini hapo akitokea jijini Arusha, baada ya kuanguka jukwaani kutokana na kuishiwa nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika, ili kumtazama katika Tamasha la Asante Tanzania.
Tukio hilo lilitokea katika tamasha hilo lililohusisha wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika  ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,  wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Baada ya kupandishwa jukwaani, alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu,”ahhh” na kisha kudondoka akiwa juu ya  jukwaa na kabla ya kutua chini, alidakwa na wasanii wenzake waliokuwa pembeni,”
Wasanii hao walimshusha jukwaani baada ya kumpumzisha kwa muda na kumtaka aende kupumzika zaidi. Akihojiwa baada ya tukio hilo, Sajuki alisema kwa sauti ya upole kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu. ”Hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana, sijisikii vizuri,”alisema Sajuki.
Haya ni maneno ya mwisho ya Sajuki kwa vyombo vya habari, wakati akiwa tayari amepitiliza siku zake za kurudi India, kuendelea na matibabu yake baada ya kukosa Sh28 milioni.
Wastara aliwahi kumwambia mwandishi wa habari hii kuwa,  Sajuki alipaswa kurejea India Desemba 6 mwaka jana, lakini alikwama kufanya hivyo kutokana na upungufu wa pesa. Hata hivyo  alisema  waliamua kuandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kutunisha mfuko wa matibabu yake.
Tamasha la kwanza la wasanii hao lilifanyika mkoani Iringa Novemba 25 mwaka jana na kupambwa na wasanii wengi wa muziki na filamu. Tamasha lingine lilifanyika Desemba 18 jijini Arusha.
Ugonjwa wa Sajuki
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu, yalipamba moto.
Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini,  mapema mwaka 2011 alipoanza kuugua. Mei mwaka 2012 alifanikiwa kwenda India kwa matibabu na baadaye  alirejea nchini na kuonekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Waongoza Filamu wa Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri, hivi karibuni, Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu,  uti wa mgongo na  kansa  ya ngozi.


Alipokuwa India kwa matibabu, Sajuki aligundulika kuwa ana ugonjwa mwingine, tofauti na ule uliompeleka kufanyiwa upasuaji.
Kwa mujibu wa Wastara, walipokuwa India (katika Hospitali ya Apollo), Sajuki alifanyiwa vipimo mbalimbali ili kubaini matatizo yanayomsumbua.
Alisema katika uchunguzi huo, ilibainika kuwa mumewe  alikuwa na  tatizo kwenye uti wa mgongo na ngozi ya mwili mzima.
Baadaye pia ilibainika kuwa alikuwa na  tatizo la pumzi, jambo lililosababisha asitibiwe ugonjwa wake ambao  kabla ya kufanyiwa operesheni, alitakiwa  kuwa katika hali ya kawaida.
Inajulikana kuwa Sajuki aliumwa na kufikia kipindi cha kudhoofu mwili jambo lililosababisha wasanii wenzake na watu wengine, kuamua kumchangia fedha ili akapate matibabu.
Wasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezi hilo na kumwezesha  kwenda India kwa mara ya kwanza Mei mwaka 2012.
Hata hivyo alikuwa hajapona sawasawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena India kwa matibabu zaidi na hili alilikiri kwenye kipindi cha ‘Mkasi’ kinachoendeshwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.
Mikasa
Sajuki ambaye ameacha mjane ‘Wastara’ aliye mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajali mwaka 2008 siku chache kabla ya ndoa yao, alikumbwa na mikasa mingi jambo lililosababisha kutokufanya sanaa yake ya uigizaji kwa ufanisi kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.
Sajuki na Wastara walipata ajali hiyo katika maeneo ya Tabata Bima, ajali iliyosababisha Wastara kupoteza mguu wake mmoja.  Hata hivyo Sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa ameshapeleka posa kwa familia ya kina Wastara.
Tukio hilo liligusa hisia za watu wengi na kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanamume mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya.
Mwananchi

Wednesday, January 2, 2013

SAJUKI KUZIKWA IJUMAA, WAZIRI FENELLA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.


 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwasili nyumbani kwa Marehemu SAJUKI Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Mke wa marehemu Wastara aliyefunikwa kanga ilikuwa ni vigumu kuamini kama mumewe kipenzi hatamuona tena alikuwa  akilia muda wote na kufarijiwa na ndugu wa karibu nyumbani kwao Tabata Bima jijini Dar. kushoto ni mama wa marehemu Bi. Zaitun

Wasanii wakiwa wamejitokeza katika msiba wa mwenzao.

Watu waliojitokeza msibani huku wengine wakiwa wamekaa kwenye mitaro ya maji.
Watu wakiwa msibani huku wakijadili mambo mbali mbali. Msiba wa Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' umewagusa wengi na kuleta simanzi.
*Marehemu Juma Kilowoko anatarajiwa kuzikwa ijumaa saa 5 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangaraamewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.

Dkt. Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.

Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ.

Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.

Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.

Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEN.
(Picha na www.elimuboratanzania.blogspot.com