Maofisa
Usalama wa Marekani, wakiingia Uwanja wa Ndgege wa Zamani, jijini Dar es
Salaam, ilikotua ndege ya Rais Barrack Obama wa Marekani kwa ajili ya
kuimarisha ulinzi uwanjani hapo jana.
Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, ni miongoni mwa Viongozi waliofika
kumpokea Rais wa Marekani Barack Obama, alipowasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Tanzania.
Ndege iliomchukuwa Rais Obama ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere
Ndege ya Rais wa Marekani, Barrack Obama, 'Airforce One' ikiwa imetua tayari, uwajani hapo.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na Balozi
wa Marekani Nchini Tanzania Balozi Alfonso, wakiende kumpokea Mgeni wao
Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili katika Uwanja wa Mwalim Nyerere
kwa ziara ya Siku mbili kutembelea Tanzania akitokea Nchini Afrika ya
Kusini.
Rais wa Marekani akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim
Nyerere kwa ziara ya siku mbili, akiongozana na Mkewe na Watoto wake
wakishuka katika ndege yake.
Rais Obama akiteta na Mwenyeji wake Rais Kikwete alipowasili Tanzania akiwa katika ziara ya siku mbili Tanzania.
Rais Obama akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete
wakielekea katika jukwaa maalum aliloandaliwa kwa ajili ya kupingwa
wimbo wa Mataifa haya mawili
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Marekani Barack Obama. wakiwa katika uwanja wa ndege.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na
Rais wa Marekani Barack Obama wakati alipowasili katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete
akimtambulisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohamed Shein kwa Rais wa Marekani Barack Obama
Makamu wa pili wa Rais , Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Rais wa
Marekani Barack Obama wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar leo
Spika wa Baraza la wawakilishi , Zanzibar Pandu Ameir Kificho
akisalimiana na Rais wa Marekani Barack Obama wakati alipowasili katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Marekani Barack
Obama, katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam jana, akiwa nchini katika ziara ya siku mbili kwa mualiko wa kiserikali.
alipowasili Uwanjani hapo kwa ajili ya
kumpokea mgeni wake, Rais wa Marekani, Barrack Obama.
Rais Barraka Obama akishuka na mtoto wake mkubwa Mallya, uwanjani
hapo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku mbili
nchini.
Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama, Michelle Obama, akishuka kwenye ndege hiyo na mtoto wake, Sasha.
Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama 'First lady' akikumbatiana na
Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo na mumewe
(kulia), leo mchana.
Rais Obama akipokea maua kutoka kwa mtoto Zakia Minja, uwanjani hapo.
Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili uwanjani hapo jana mchana.
Rais Obama akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21.
Rais Obama akitoka kukagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara
baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21, uwanjani hapo jana.
Rais Barrack Obama akiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete
akipokea gwaride la heshima uwanjani hapo, mara baada ya kuwasili jana
mchana.
Rais Barrack Obama akisalimiana na mke wa Rais Kikwete, Mama Salama mara baada ya kupokea gwaride la heshima uwanjani hapo.
Rais Barrack Obama, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Hapa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Akisalimiana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.
Hapa Rais Obama na mwenyeji wake, Rais Kikwete, wakifurahia ngoma ya Mganda ya asili ya Wangoni, mkoani Songea.
Hapa Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuondoka Uwanja wa ndege.
Wananchi wakiwa wamekusanyika nje ya jengo la Ikulu kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama.
Wananchi waliokusanyika nje ya jengo la Ikulu jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama,wakipunga bendera za
Tanzania na Marekani.
Maofisa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwa nje ya Ikulu, kumkaribisha Rais,
Barrack Obama.
Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma (kulia), akiwa na mgeni wake, First lady, Michelle Obama, kwenye Ofisi za Wama.
Hapa wakiwa Makumbusho ya Taifa, wakipokea mau kwa ajili ya kuweka
kwenye mabaki ya vifaa vilivyolipuliwa na bomu kwenye Ubalozi wa
Marekani jijini Dar es Salaam.
Wake hao wa Marais wa Marekani na Tanzania, wakiweka mashada hayo
kwenye mabaki hayo kwa ajili ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao
kwenye tukio hilo.
Wakiwaombea wahanga hao, mara baada ya kuweka mashada hayo ya maua.
Rais Obama Akionyesha Shoo ya Kabumbu Ubungo
|
Rais
Jakaya Kikwete wa Tanzania akimpasia mpira Rais Barack Obama wa
Marekani leo kama sehemu ya kuonyesha uwezo wao kisoka pia |
Hapa Rais Obama akionyesha ujuzi katika soka eneo la Ubungo
Rais Jakaya Kikwete kulia akimtazama Rais wa Marekani Barack Obama akionyesha uwezo wake katika soka eneo la Ubungo leo
Mbali ya kuwa Rais wa dunia pia katika soka yumo Rais Obama
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mwenyeji wake Rais Barrack Obama wa
Marekani wakipata maelezo juu ya kituo cha uzalishaji wa Umeme Ubungo
kinachoendeshwa na kampuni ya symbion power wakati viongozi hao
walipofanya ziara katika kituo hicho leo asubuhi.Watatu kushoto ni
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Symbion Power Bwana Paul Hinks(picha na
Freddy Maro)
Serikali
ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki
kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan
chi hizo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye
hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili
nchini Tanzania.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za
afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano
wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
“Sasa
ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani ili
kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema
Rais Obama.
Aliongeza
kuwa pia ushirikiano huo unapaswa kuboresha utoaji wa mizigo katika
bandari ya Dar es salaam na Mombasa kwenda nchi zisizo na bandari ili
kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini.
Akizungumzia
hotuba ya Rais Obama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini
(CTI) Felix Mosha alipongeza hotuba hiyo kwa kufungua ukurasa mpya kwa
nchi za Afrika na Marekani kwa kuonyesha kuwa wakati wa kutegemea
misaada umepitwa na wakati badala yake ni kushirikiana katika uwekezaji.
Katika mkutano huo kiasi cha wafanyabiashara 170 walihudhuria mkutano huo
picha na habari kwa hisani ya Zenjinews; Kassim
Mbarouk-www.bayana.blogspot.com na Francis Godwin Mzee wa matukio