Klabu ya
Azam FC imeanza rasmi maandalizi ya kutetea ubingwa wao msimu ujao na
michuano ya kimataifa kwa kukamilisha usajili wa mchezaji wa kimataifa
wa Burundi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Yanga.
Taarifa rasmi zilizothibitishwa na
meneja wa Azam FC Jemedari Said ni kwamba mshambuliaji Didier Kavumbagu
amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
“Ni kweli Kavumbagu tumemalizana nae na amesaini mkataba wa mwaka mmoja. Taarifa zaidi zitatolewa baadae.” Alikaririwa Jemedari.
Kavumbagu alitua nchini Tanzania
akitokea Burundi alipokuwa anaitumikia Vital O na kuja kujiunga na Yanga
misimu miwili iliyopita.(Awadh Ibrahim)
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment