
Ndugu zangu,
Inasemwa, kuwa Mungu alimuuliza Mussa; " Umeshika nini mkononi?"
Naye Mussa akajibu; " E baba, nimeshika fimbo tu!"
Mungu akamwambia Mussa;
" Yatosha sana kuwakombolea Wana-Israel kutoka kwenye nchi ya Misri"
Naye Mussa akajibu; " E baba, nimeshika fimbo tu!"
Mungu akamwambia Mussa;
" Yatosha sana kuwakombolea Wana-Israel kutoka kwenye nchi ya Misri"
Na hakika, kwa mwanadamu, kila ulichonacho mkononi chatosha kabisa kufanya makubwa maishani mwako.
Yumkini wengine hatuna fedha mifukoni
za kutosha kugawa kwa wengine wenye kuhitaji, lakini, na tuamini, kuwa
hata yale machache tuliyonayo vichwani mwetu, yatosha kabisa kuwakomboa
wanadamu wenzetu wenye kutaabika na waliozama kwenye lindi la umasikini.
Ni Neno Fupi La Usiku. ( Pichani
nikizungumza na akina mama wa umoja wa wakulima na wajasiri amali
Mbarali, ujulikanao kama UWAKIUMBA, Chimala, Leo asubuhi.)
Maggid Mjengwa,
Iringa.
Iringa.
No comments:
Post a Comment