
Nzega. Zaidi ya magari 1,000 yamekwama
kwenye Barabara Kuu ya Mwanza - Dar es Salaam katika Kijiji cha Ngonho,
Kata ya Miguwa, wilayani Nzega, kutokana utekaji wa malori uliofanywa
juzi usiku. (JM)
Kutokana na tukio hilo, waligoma
kuondoa magari yao na kusababisha mabasi ya abiria na malori ya mizigo
kukwama wakati abiria wapatao 3,000 wakitaabika kwa kukosa chakula na
maji.
Madereva hao waligoma kuondoa magari
yao baada ya kukasirishwa na kitendo cha polisi wa Nzega kushindwa
kuwasaidia wakati walipotekwa.
Madereva hao wameapa kutoondoa magari
hayo hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias
Chikawe au Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa watakapofika kwenye eneo
hilo ili kusikiliza kilio chao.
Unyama wa watekaji
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya
Wilaya ya Nzega, Emmanuel Mihayo alisema watu walijeruhiwa vibaya kwenye
utekaji huo kwa kukatwa masikio na kutobolewa macho.
Dk Mihayo aliwataja majeruhi hao kuwa
ni raia wa Burundi, Herelina Eddy, ambaye alitobolewa macho na hali yake
ilikuwa mbaya na alikuwa kwenye maandalizi ya kupelekwa Hospitali ya
Rufaa ya Nkinga kwa matibabu zaidi.
Alisema majeruhi wengine wawili
wanaendelea vizuri na matibabu katika hospitali hiyo. Majeruhi hao ni
Abraham Ismail na Omary Adrian, ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam.
Alisema Adrian alikatwa sikio na shavu pamoja na mkono wa kushoto wakati Ismail alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.
Polisi watuhumiwa
Mmoja wa madereva waliotekwa, ambaye
aliomba jina lake kuhifadhiwa alisema kuwa polisi wa Nzega waliombwa
kutoa msaada lakini walikataa. CHANZO
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment