Mapendekezo yaliyowasilishwa
na Jaji Warioba hayakuwa maoni yake, yale ni maoni ya wananchi,
Tanganyika imevaa koti la Muungano, ametoa ushahidi wake ili kujenga
mwafaka katika kuendeleza Muungano wenye mfumo wa serikali tatu,"
Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif
Hamad amesema chama chake cha CUF hakiko tayari kujadili mfumo wa
Muungano wa serikali mbili kama inavyotetewa na wabunge wa CCM na Rais
Jakaya Kikwete.
Amesema tayari amewaandikia barua Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwaeleza juu ya msimamo huo.
Maalim Seif alitoa msimamo huo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.(Hudugu Ng'amilo)
Isitoshe,
alisema CUF imebaini kuwa kuna njama za kufuta kipengele katika Katiba
ya Zanzibar kinachosema; "Zanzibar ni nchi" na kwamba hiyo ni sawa na
kutwanga maji kwenye kinu kwa kuwa Wazanzibari kamwe hawatakubali
kufanya hivyo.
Maalim
Seif alisema haikuwa mwafaka kwa Rais Kikwete kukosoa mapendekezo ya
Rasimu ya Katiba yanayotaka mfumo wa Muungano kuwa wa serikali tatu.
Alisema
Jaji Warioba aliweka kando itikadi yake ya CCM katika utendaji wake
kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuja na uamuzi huo kwa vile ndiyo
tiba ya kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
"Mapendekezo
yaliyowasilishwa na Jaji Warioba hayakuwa maoni yake, yale ni maoni ya
wananchi, Tanganyika imevaa koti la Muungano, ametoa ushahidi wake ili
kujenga mwafaka katika kuendeleza Muungano wenye mfumo wa serikali
tatu," alisema Maalim Seif.
Alisema
Muungano wa serikali mbili hauvumiliki na kama kuna watu wanaendelea
kuutetea mfumo huo, Zanzibar inaweza kutumia sheria yake ya kura ya
maoni kuwauliza wananchi wanaotaka na wasiotaka jambo hilo.
"Nimemwandikia
barua Rais Kikwete, nakala nimempelekea Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed
Shein, Tanzania Bara wanataka Zanzibar iondoe kifungu cha Katiba
kinachosema Zanzibar ni nchi, jambo hilo halitapita...tutafanya kampeni
wananchi walikatae," alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF.
Alisema
ni jambo la kusikitisha katika hotuba yake alijisahau kama ni mkuu wa
nchi na analihutubia Bunge Maalumu badala yake akaegemea kuwa mwenyekiti
wa CCM.
Alisema
haikuwa sahihi kutoa vitisho na kutaja ikiwa Serikali ya Muungano chini
ya Serikali tatu italegalega, jeshi litachukua madaraka ya nchi.
"Rafiki
na ndugu yangu Kikwete, usifikiri huu ni wakati ule wa Julius Nyerere,
akisema yeye hakuna wa kumpinga. Mambo yamebadilika, usijifanye ni
Nyerere mpya, hakuna atakayekusikiliza na kubabaika," alisisitiza Maalim
Seif.Alisema ikiwa viongozi wa Muungano wanajiandaa kutisha watu na
kusababisha ghasia katika nchi, mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai
ipo na watakaosababisha fujo na umwagaji wa damu watafikishwa mbele ya
mikono ya sheria bila ya kujali nyadhifa na madaraka yao.
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment