Saturday, March 21, 2015

BREAKING NEWZZZZZ: ZITTO KABWE AJIUZULU RASMI UBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI USIKU HUU BUNGENI DODOMA

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa Tiketi ya Chadema, Kabwe Zitto akisoma barua aliyomwandikia Spika wa Bunge, Anne Makinda kumtaarifu kuwa anang'atuka nafasi ya Ubunge. Pia aliwaaga Wabunge wenzake na kuahidi kurudi tena Mungu akijalia baada ya Uchaguzi wa mwaka huu.
Wabunge mbalimbali wakiwepo wa Chadema, Cuf, NCCR na CCM walionekana dhahiri kububujikwa na machozi kufuatia kujivua kwake Ubunge.

HII NDIO BARUA ALIYOISOMA BUNGENI 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe usiku huu ametangaza rasmi Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria 
ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba anategemea kuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu.CHANZO :  MTAA KWA MTAA BLOG

No comments:

Post a Comment