Monday, March 16, 2015

KARDINAL PENGO AWAKOSOA MAASKOFU JUU YA KURA YA HAPANA KATIBA MPYA

UFUATAO ni ujumbe mfupi wa Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alioutoa leo katika Kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam kuhusiana na waraka wa maaskofu uliotolewa hivi karibuni kwa Wakristo nchini kujiandikisha kikamilifu na kisha kuikataa Katiba Inayopendekezwa wakati wa kura ya maoni kwa vile haikujadiliwa kiuadilifu.
"Maaskofu hatuna mamlaka ya kuwaamulia/kuwalazimisha waumini wetu wafanye uamuzi gani kuhusu katiba, kuwaamulia ni kuwadharau kuwa hawawezi kufanya uamuzi sahihi wao wenyewe na kuingilia uhuru wao.
Waraka huu unaleta utengano katika taifa kuwa Wakristo, tumechukua uamuzi dhidi ya serikali na wengine....

Tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa tafakari yao binafsi bila shinikizo letu.....

Wakati hili linajadiliwa nilikuwa Italy katika kusimikwa makardinali na baadaye India, wengine wakavumisha nimelazwa,..wengine nimefariki, lakini namshukuru Mungu hizo ni dua za kuniongezea maisha marefu na afya (makofi).

Nililetewa waraka nikausoma, umepitishwa baada ya tafakari kubwa nauheshimu. Lakini nadhani tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa uhuru baada ya kutafakari....

Si sahihi tukaenda katika katiba kama Wakristo kwa shinikizo la kupinga katiba...

Wawe huru anayepinga kwa hiari yake anayekubali kwa dhamiri yake....
Sidhani kama viongozi wa dini sasa tuna amri ya kulazimisha uamuzi juu ya katiba....

source: vijana na Matukio

No comments:

Post a Comment