Monday, May 27, 2013

WANATETA NINI HAPA?

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Inkhosikati La-Ntentesa, Mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland

INAPENDEZA VIONGOZI WETU WAKUU WAKIFURAHI PAMOJA:


h 86c68
  JK AKUTANA NA MARAIS WASTAAFU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizingumza na Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim kuhusiana na sherehe za miaka 50 ya AU alipokutana nao jijini Addis Ababa, Ethiopia

source: mjengwa blog

Wednesday, May 22, 2013

Jana, Wabunge wetu almanusura wawe mabondia nje ya Bunge

via gazeti la MTANZANIA, Mei 21, 2013: Baada ya Bunge kuahirishwa, nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri baina ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu.

Maneno hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia Lissu.

Tuesday, May 21, 2013

Tukichoka kuhubiri amani, tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi - Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Naiona hatari kubwa nyingine inakuja mbele yetu. Ni haya makundi mawili; MaBodaboda na MaMachinga. Hofu yangu kuna wanasiasa wachache wanaowaona vijana hawa, katika matatizo yao ya kiuchumi, kuwa ni mtaji wa kisiasa. Na kimsingi wanawageuza kuwa ' Shuka za Kisiasa'. Na hapa ni wanasiasa wa vyama vyote.

Hatari yake?
Viongozi wasipokuwa makini, wakaacha kutanguliza busara na hekima kwenye kauli zao, basi, hofu ya kauli kupelekea machafuko na kuvunjika kwa amani itabaki kuwepo.

Maana, hawa MaBodadoba na MaMachinga, pamoja na kuwa wengi wao ni vijana wema kabisa, na ambao, kwenye mahangaiko yao, kama wagonjwa, wanamsikiliza kila anayekuja na kauli za kuwapa matumaini, hata kama ni ya muda mfupi,  na hata kama ni kwa kuvunja sheria.

Na kwa vile Elimu ya Uraia iko chini sana katika jamii yetu, hata kwa miongoni mwa viongozi wetu, basi, ndio maana naiona hatari hii kubwa inayokuja mbele yetu. Kwamba MaBodaboda na MaMachinga wakiendelea kutumiwa kama ' Shuka za Wanasiasa', basi, yumkini, huko tuendako Watanzania tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi.

Maana, siku zote, maovu huzaa maovu. MBodaboda au Mmachinga mmoja akiuawa, kuna mia watakaokuja kutaka kulipiza kisasi. Na Polisi mmoja akiuawa, kuna operesheni ya kipolisi itakayofuata. Na polisi wetu hawa ni vijana hawa hawa ambao wengine wameponea chupuchupu kuwamo  kwenye makundi haya ya MaBodaboda na MaMachinga, lakini sasa, tumewapa pia silaha za moto wabebe.

Naam, tukichoka kuhubiri Amani, Upendo Na Mshikamano, basi, tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi.

Maggid
Iringa

Taswira:Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay Ajiunga Rasmi na Chadema Leo

 The heavy weight MC Proj Jay, aka Dady, Joseph Haule akipokea Kadi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu Muda mfupi uliopita Mjini Dodoma Mara baada ya kujiunga rasmi na Chadema
Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu
Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema John Mnyika(kulia)akiteta jambo na mbunge wa mbeya mjini-Chadema Joseph Mbilinyi aka Sugu muda mfupi baada ya Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay kujiunga na chadema leo Mjini Dodoma
--

Muda si mrefu msanii maarufu hapa Bongo Profesa Jay (Joseph Haule) amejiunga na Chama Cha Demokrasi na Maendeleo huko Dodoma na amekabidhiwa tiketi ya chama cha CHADEMA rasmi na Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi aka Sugu huko Dodoma

source: haki ngowi

Thursday, May 16, 2013

DR. SLAA VS NAPE NNAUYE

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akisalimiana na kufurahia jambo na Katibu Mwenezi wa CCM Nape Moses Nnauye walipokutana katika Studio za ITV.Picha na Chadema
 
source Haki Ngowi

Akina dada mmeambiwa mfuate mfano huu wa Mwanjelwa kwa Mwakyembe huko Bungeni

Picture
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Dk Mary Mwanjelwa Bungeni mjini Dodoma, Mei 13, 2013. (Picha na Edwin Mjwahuzi)

Monday, May 13, 2013

Taswira:Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Msanii Mrisho Mpoto

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na msanii Mrisho Mpoto wakati alipozindua kampeni ya Made in  Tanzania  inayowahamasisha vijana kutumia fursa zilizopo nchini  kuzalisha bidhaa,  iliandaliwa na Kampuni ya Clouds FM Group kwenye uwanja Nyerere Mjini Dodoma Mei 12, 2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
source: haki ngowi

Friday, May 10, 2013

Taswira Katika Taifa:Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Akifurahia Jambo na Mbunge wa Singida Mashariki-Chadema, Tundu Lissu




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Singida  Mashariki-Chadema, Tundu Lissu kwenye uwanaj wa ndege wa Kilimanjaro alikowasili  May 8,2013 ili kufungua mkutano Mkuu wa ALAT jijini Arusha, May 9, 2013. Lisu pamoja na wabunge wengine walikwenda Arusha kujionea athari za mlipuko wa bomu kwenye Kanisa Kstoliki la Olasiti.Katikati ni Mbunge wa Igalula  Athumani Mfutakamba.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

source: Haki Ngowi

Saturday, May 4, 2013

saba wafa papo hapo, zaidi ya 50 wajeruhiwa ajali ya taqwa,nyololo

 
tagwa2 23791 

WATU saba wamekufa papo  hapo na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari  matatu tofauti katika barabara kuu ya Iringa-Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea jana jioni eneo la Nyololo wilayani Mufindi.  Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni Scania lenye No T 104  BZZ lililokuwa limebeba Trella No T 309 BTS mali ya Kampuni ya Sogea Sotom ya Dar-es-salaam lilikuwa likilipita gari aina ya Nissan bus No T 273 CBR mali ya kampuni ya TAQWA wa Dar-es-salaam lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Malawi.
Scania hiyo iligonganga uso kwa uso na Scania nyingine yenye namba za usajili  T 597 AMZ  likiwanaTrella T227 AVK mali ya Nyato wa Dar-es-salaam.


Majina ya waliokufa katika ajali hiyo ni Abrahiman Abdul (32) dereva wa basi la Taqwa mkazi wa Dar es Salaam, Nassoro Rashid (27) kondakta mkazi Tanga, Shaen Ramadhani (32) mkazi wa Dar es salaam, Ally Suleman (26) mfanyabiashara wa Dar Es Salaam na wengine watatu majina yao hayajafahamika.

Alisema majeruhi hao wamefikishwa katika hospitali ya Mafinga kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

source: mjengwa Blog

Kauli za Bungeni zilizowaacha Wananchi na vijiulizo

"Kaa chini, mbona unawashwawashwa... Kaa chini. Usitafute umaarufu hapa..." Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba (CCM) akimnyamazisha John Mnyika, Mbunge wa Ubungo (CHADEMA).

"Kwa kuwa wanaume wengi wanabaka, kifunguliwe kituo wafundishwe kutongoza.” Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Leticia Nyerere.

‘‘Kuna wabunge ambao wana mimba sizizotarajiwa Bungeni...” Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde.

“Sikufurahishwa na kauli ya Lusinde kwamba tuna mimba sizizotarajiwa.”  Anna Abdallah (Viti Maalum, (CCM).

“UDOM (Chuo Kikuu cha Dodoma) kuna udini wa hali ya juu, wanafunzi wa dini tofauti hawalali chumba kimoja.”
Mbunge wa Rombo (CHADEMA), Joseph Selasini.

“Serikali ina tatizo kwa kuwa kuna akili ndogo inatawala vichwa vikubwa.” Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa.

‘‘Siongei na mbwa bali naongea na mwenye mbwa.” Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM), Juma Nkamia

‘‘Mambo mengi nchi hii hayaendi kutokana na serikali pumbavu, hatuwezi kuwa na waziri wa elimu boya...”
Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA, Joseph Mbilinyi.

“Serikali iruhusu raia wa Tanzania walime bangi wapate fedha za kigeni.” Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Keissy.

Wednesday, May 1, 2013

hongera magufuli

21 f424b
Hapa ni Mkoa wa Singida, kwa hakika uzuri wa Barabara hii ni ushahidi wa usimamazi mzuri wa waziri mwenye dhamana.

source: mjengwa blog