Saturday, May 4, 2013

saba wafa papo hapo, zaidi ya 50 wajeruhiwa ajali ya taqwa,nyololo

 
tagwa2 23791 

WATU saba wamekufa papo  hapo na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari  matatu tofauti katika barabara kuu ya Iringa-Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea jana jioni eneo la Nyololo wilayani Mufindi.  Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni Scania lenye No T 104  BZZ lililokuwa limebeba Trella No T 309 BTS mali ya Kampuni ya Sogea Sotom ya Dar-es-salaam lilikuwa likilipita gari aina ya Nissan bus No T 273 CBR mali ya kampuni ya TAQWA wa Dar-es-salaam lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Malawi.
Scania hiyo iligonganga uso kwa uso na Scania nyingine yenye namba za usajili  T 597 AMZ  likiwanaTrella T227 AVK mali ya Nyato wa Dar-es-salaam.


Majina ya waliokufa katika ajali hiyo ni Abrahiman Abdul (32) dereva wa basi la Taqwa mkazi wa Dar es Salaam, Nassoro Rashid (27) kondakta mkazi Tanga, Shaen Ramadhani (32) mkazi wa Dar es salaam, Ally Suleman (26) mfanyabiashara wa Dar Es Salaam na wengine watatu majina yao hayajafahamika.

Alisema majeruhi hao wamefikishwa katika hospitali ya Mafinga kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

source: mjengwa Blog

No comments:

Post a Comment